Siku ya Mtoto wa Afrika

Machafuko ya Soweto ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika

Siku ya Mtoto wa Afrika (kwa Kiingereza: Day of the African Child) ni siku inayosherehekewa kila mwaka tarehe 16 Juni tangu mwaka 1991 ilipoteuliwa na Umoja wa Afrika katika kuenzi michango ya watoto walioshiriki katika maandamano katika mji wa Soweto, Afrika Kusini mwaka 1976 pamoja na kujengea jamii uelewa juu ya umuhimu wa elimu bora kwa watoto.

Tarehe 16 Juni 1976, maelfu ya watoto katika nchi ya Afrika Kusini walikusanyika katika mji wa Soweto kwa ajili ya maandamano yenye malengo ya kudai elimu bora, mamia ya watoto walipigwa risasi na kuuliwa, watoto zaidi ya elfu moja walijeruhiwa.

Tarehe 16 ya kila mwaka, mataifa, jumuia mbalimbali na jumuia za kimataifa pamoja na wadau mbalimbali hukusanyika pamoja kwa ajili ya kujadili fursa na changamoto zinazowakumba watoto katika bara la Afrika.

Viungo vya Nje

hariri