Soweto

mji wa Afrika Kusini

Soweto ni sehemu ya jiji la Johannesburg, Afrika Kusini.

Soweto.
Mtaa wa vibanda katika Soweto.
Nyumba alipokaa Nelson Mandela 1946 - 1962 pale Soweto, Vilakazi Street.

Jina hilo ni kifupi cha Southwestern townships yaani "mapambizo ya kusini-magharibi". Hayo yalianzishwa wakati wa apartheid kama makazi ya Waafrika pekee, na kwa hiyo yalitazamwa kuwa "mapambizo meusi" ya Johannesburg.

Kati ya miaka 1983 na 2002 Soweto ilikuwa manisipaa ya pekee, baadaye imekuwa tena sehemu ya jiji la Johannesburg.

Wakati wa sensa ya mwaka 2008 idadi ya wakazi ilikuwa milioni 1.3 [1] na hii inalingana na theluthi moja ya wakazi wote wa jiji hilo.

Ndani ya Soweto kuna vitongoji mbalimbali, idadi inatajwa mara kuwa 29[2], mara 34[3]. Kati yake, vingine ni maeneo maskini sana, hata mitaa ya vibanda; vingine vina nyumba nzuri.

Soweto ilikuwa kitovu cha upinzani wa wanafunzi dhidi ya apartheid kwenye mwaka 1976.

Tanbihi Edit

  1. Population of Soweto, South Africa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2019-09-17.
  2. Soweto, tovuti ya saweb.co.za, iliangaliwa Septemba 2019
  3. Background to the study area: Soweto. University of Pretoria (2004). Iliwekwa mnamo 2009-11-16.

Kujisomea Edit

Viungo vya Nje Edit

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Soweto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.