Sikusare machipuo

Sikusare machipuo (pia ikwinoksi machipuo[1], ing. vernal equinox) ni moja ya sikusare mbili za mwaka yaani siku ya usawa wa muda wa mchana katika maeneo mbali ya kanda ya ikweta.

Sikusare machipuo ni sikusare ambako kipindi cha usiku mrefu umekwisha na kipindi cha nusu mwaka kinaanza ambako mchana ni mrefu kuliko usiku. Kuongezeka wa muda wa mchana kunasababisha kupanda kwa halijoto hivyo katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuotea majani mapya.

Sikusare ya machipuo inakadiriwa kuwa 21 Machi kwenye nusutufe ya kaskazini na 23 Septemba kwenye nusutufe ya kusini.

Katika kalenda ya Kiajemi (Iran, Afghanistan, Tajikistan) ni sikukuu inayoitwa Noruzi (نوروز‎ nowruz, pia Nauruzi) na kuwa mwanzo wa mwaka mpya ya Kiajemi.

  1. kutoka Kiingereza-Kilatini "equinox"; KAST inatumia "sikusare", TUKI-ESD "ikwinoksi"