Simon Nkoli

mwanaharakati (1957-1998)

Simon Tseko Nkoli (26 Novemba 1957 - 30 Novemba 1998) alikuwa mpinzani wa ubaguzi wa rangi, mdai haki za mashoga na mwanaharakati wa UKIMWI wa Afrika Kusini.

Mwanaharakati shoga Simon Nkoli

Maisha hariri

Nkoli alizaliwa Soweto katika familia inayozungumza SeSotho. Alikulia kwenye shamba huko Free State na familia yake, baadaye ilihamia Sebokeng. Nkoli alikua mwanaharakati wa vijana dhidi ya ubaguzi wa rangi, akiwa na Baraza la Wanafunzi wa Afrika Kusini (COSAS) na United Democratic Front.

Mnamo mwaka 1983, alijiunga na Chama cha Mashoga cha Afrika Kusini (kilichounganisha hasa Wazungu), kisha akaunda Kikundi cha Jumamosi, kikundi cha kwanza cha mashoga Weusi barani Afrika.

Nkoli alihotubia mikutano ya hadhara ya kuunga mkono kugomewa kwa kodi za nyumba katika mitaa ya watu weusi. Mnamo mwaka 1984 alikamatwa akashtakiwa kutenda uhaini na kutishiwa na adhabu ya mauti pamoja na viongozi wengine 21 wa kisiasa katika Kesi ya Uhaini ya Delmas, ikiwa ni pamoja na Popo Molefe na Patrick Lekota, wote kwa pamoja wanajulikana kama Delmas 22. Aliachiliwa huru na kutolewa gerezani mnamo mwaka 1988. Kwa kuwa wazi kuliko hali yake ya mshoga akiwa mfungwa, alisaidia kubadilisha mtazamo wa African National Congress kwa haki za mashoga.

Alianzisha Shirika la Mashoga na Wasagaji la Witwatersrand (GLOW) mnamo mwaka 1988.[1] Pamoja na mwanaharakati wa LGBT, Beverley Palesa Ditsie, aliandaa onyesho la kwanza lijulikanalo kama gwaride la kujivunia nchini Afrika Kusini lililofanyika mnamo 1990.[2] Alisafiri sana na alipewa tuzo kadhaa za haki za binadamu huko Ulaya na Amerika Kaskazini. Alikuwa mwanachama wa bodi ya Chama cha Kimataifa cha Washoga na Wasagaji, akiwakilisha eneo la Afrika.

Alikuwa mmoja wa wanaharakati wa kwanza wa mashoga kukutana na Rais Nelson Mandela mnamo mwaka 1994. Alisshiriki katika kampeni ya kuingiza kinga dhidi ya ubaguzi wa kijinsia katika Orodha ya Haki za Binadamu kwenye Katiba ya Afrika Kusini ya 1994. Alishiriki pia katika kampeni ya kufuta sheria ya ulawiti iliyofanyikiwa Mei 1998.

Baada ya kuwa kati ya washoga Waafrika wa kwanza waliokiri hadharani kuambukizwa VVU, alianzisha kikundi Positive African Men (Wanaume Chanya wa Kiafrika) mjini Johannesburg. Aliishi na VVU kwa karibu miaka 12, na na miaka minne ya mwisho maishani mwake alikuwa akiumwa vibaya, akiwa na vipindi vya kujisikia nafuu.. Alikufa kwa UKIMWI mnamo mwaka 1998 huko Johannesburg.

Kuna siku ya kumbukumbu ya Simon Nkoli huko San Francisco, Marekani. Alifungua Michezo ya Mashoga ya kwanza huko New York akapewa tuzo ya heshima ya jiji hilo na meya David Dinkins. Mnamo mwaka 1996 Nkoli alipokea Tuzo ya Stonewall katika Royal Albert Hall huko London. Msanii wa filamu wa Kanada John Greyson alitengeneza filamu fupi kuhusu Nkoli iliyopewa jina la "A Moffie Called Simon" mnamo mwaka 1987.[3] Nkoli alikuwa mhusika katika tamthilia ya Robert Colman wa 2003, "Your Loving Simon" na filamu ya Beverley Ditsie ya 2002 "Simon & I".[4] Filamu ya John Greyson ya 2009 "Fig Trees", maandishi / opera ya mseto ni pamoja na kumbukumbu ya uanaharakati wa Nkoli.[5]

Marejeo hariri

  1. Hoad, Neville Wallace; Martin, Karen; Reid, Graeme, wahariri (2005). Sex and Politics in South Africa. Cape Town: Double Storey. ku. 30–31,169,191,239. ISBN 9781770130159. 
  2. Mohlamme, Charity (2006). "It Was Part Of Our Coming Out...". Katika de Waal, Shaun; Manion, Anthony. Pride: Protest and Celebration. Fanele. uk. 36. ISBN 978-1-77009-261-7. 
  3. Botha, Martin (2002), "Homosexuality and South African Cinema", Kinema (Spring 2002), ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 August 2006  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  4. "Bev and Simon: a South African 'love story'", Radio Netherlands Archives, January 23, 2004
  5. "Canadian filmmaker John Greyson Turns Down Offer to Appear at Israeli Film Festival", Imoovizine, 2009-04-11, ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 July 2009  Unknown parameter |df= ignored (help); Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Simon Nkoli kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.