Makala hii inataja Mnara kama jengo refu. Kwa makala ya Mnara kata ya Wilaya ya Lindi Vijijini, tafadhali fungua hapa.

Mnara wa Eiffel ni ishara ya mji wa Paris.

Mnara (kut. Kar. مناره‎ manara) ni jengo refu na kimo chake kinazidi kipenyo chake mara kadhaa.

Kuna aina nyingi za minara:

  • - siku hizi nyumba katika kitovu cha miji mikubwa hujengwa kama maghorofa yenye ghorofa makumi hadi mamia
  • - misikiti na makanisa huwa na minara kwa ajili ya matangazo ya ibada kwa njia ya sauti ya mtu au kengele
  • - minara mirefu hujengwa kwa kusudio la kupata mahali pa juu pa antena ya TV, redio au simu
  • - kwenye pwani za bahari kuna minara ya taa inayoongoza meli wakati wa usiku
  • - kuna minara ya maji inayobeba tangi kubwa ya maji katika maeneo pasipo milima kwa kusudio la kuwa na shindikizo la kudumu kwa ajili ya maji ya bomba
  • - aina mbalimbali zimejengwa kwa ajili ya kusudio maalamu kama vile mnara ambako walinzi moto hukausha mipira ya maji, minara ya parachuti ambako wanafunzi wanafanya mazoezi ya kwanza, minara ya kubeba madaraja na mengine
  • minara nyingi za kihistoria ina kusudi la ulinzi na usalama kwa mfani minara mingi ya ukuta wa China.

Mnara wa kihistoria unaojulikana zaidi ni mnara wa Babeli unaotajwa katika Biblia (kitabu cha Mwanzo 11). Wataalamu wengi huona ilikuwa aina ya zigurat yaani jengo kubwa lililounganisha tabia za mnara na piramidi.

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.