Nguva
Nguva | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nguva wa kawaida
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 2, jenasi 3 na spishi 5:
|
Nguva ni wanyama wakubwa wa oda Sirenia wanaoishi baharini. Hata hivyo ni mamalia wanaozaa watoto walio hai na kuwalisha kwa maziwa. Nguva huwa na mikono ya mbele na mkia wenye umbo la pembetatu. Wanaishi kwenye pwani za Bahari ya Hindi, Bahari ya Karibi, Afrika ya Magharibi na mto wa Amazonas. Wanaweza kufikia urefu wa mita 2.5 hadi 4 na uzito wa kg 1,500.
Wanahatarishwa kutokana na uwindaji hivyo wanalindwa kila nchi.
Jina la Kisayansi Sirenia linatoka na neno la Kigiriki Σειρῆνες Seirēnes. Neno la "nguva" pia ina maana ya mtu mwenye mwili wa mwanamke na mkia wa samaki kama sireni wa mitholojia ya Kigiriki. Hula manyasi ya bahari na mimea ya maji mingine.
Spishi
hariri- Dugong dugon, Nguva wa Kawaida (Dugong)
- Hydrodamalis gigas, Nguva Mkubwa wa Steller (Steller's Sea Cow) imekwisha sasa (mnamo 1768)
- Trichechus inunguis, Nguva wa Amazonas (Amazonian Manatee)
- Trichechus manatus, Nguva wa West Indies (West Indian Manatee)
- Trichechus m. latirostris, Nguva wa Florida (Florida Manatee)
- Trichechus m. manatus, Nguva wa Karibi (Antillean Manatee)
- Trichechus senegalensis, Nguva Magharibi (African Manatee)
Picha
hariri-
Nguva wa Amazonas
-
Nguva wa Karibi
-
Nguva magharibi
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.