"So Sick" ni wimbo wa mwimbaji wa muziki wa R&Bpop wa Kimarekani-Ne-Yo. Wimbo ulitayarishwa na watayarishaji wa Kinorwei maarufu kama Stargate kwa ajili ya albamu ya kwanza ya In My Own Words.

“So Sick”
“So Sick” cover
Single ya Ne-Yo
kutoka katika albamu ya In My Own Words
Imetolewa 26 Machi 2006
Muundo 12" single, CD single, digital download
Imerekodiwa Julai 2005
Aina R&B
Urefu 3:27
Studio Def Jam
Mtunzi M. Eriksen, T. Hermansen, S. Smith
Mtayarishaji Stargate
Mwenendo wa single za Ne-Yo
"Stay"
(2005)
"So Sick"
(2006)
"When You're Mad"
(2006)

Wimbo huu ulitoka ukiwa kama wimbo wa pili kutoka katika albamu hiyo ya In My Own Words. Hii ilifanya vyema katika chati za muziki duniani, kwa kufikia namba moja katika Marekani na Uingereza. Na pia ndiyo kibao pekee cha Ne-Yo kilichofanya vyema dunia nzima.

Video yake

hariri

Video ya wimbo huu wa "So Sick", uliongozwa na Bw. Hype Williams, imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa sana katika BET na MTV. Video mbili zilipigwa kwa ajili ya wimbo huu. Toleo halisi la video hii ilishia ikiwa bado na marekebisho kadha wa kadha. Toleo jipya la video ya wimbo huu linaonekana kupigiwa wakati wa baridi kali na ilipigiwa katika milima ya theluji.

Chati Nafasi iliyoshika
Australian Singles Chart 4
Austria Singles Chart 21
Belgium Singles Chart 17
Dutch Singles Chart 15
French Singles Chart 11
German Singles Chart 11
Irish Singles Chart 2
UK Singles Chart 1
U.S. Billboard Hot 100 1
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks 3
U.S. Billboard Pop 100 1
Swiss Singles Chart 5
Denmark Singles Chart 10
Norway Singles Chart 10
Italy Singles Chart 27

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri