Chris Rock

Mchekeshaji, mwigizaji, mwandishi, mtayarishaji wa televisheni, mtayarishaji wa filamu, na mkurugenzi wa nchini Marekan


Chris Rock (alizaliwa Georgetown, South Carolina, Februari 7, 1966) ni mchekeshaji maarufu katika nchi ya Marekani. Anajulikana kama “stand-up comedian” kwa vichekesho yake kuhusu ubaguzi wa rangi. Chris Rock ni mwigizaji, mwandishi, mtayarishaji na mwongozaji wa filamu pia[1].

Chris Rock

Amezaliwa Rosalie na Julius Rock
Februari 7 1966
Georgetown
Nchi South Carolina
Kazi yake mchekeshaji,Mwongozaji wa filamu

Maisha ya zamani hariri

Christopher Julius Rock ni jina lake kamili alilopewa na wazazi wake Rosalie na Julius Rock. Mama yake alikuwa mwalimu wa watu wenye udhaifu wa akili. Baba yake alikuwa dereva wa gari na mtu wa kutoa magazeti. Baada ya yeye kuzaliwa, wazazi wake walihamia Brooklyn, jimbo la New York. Chris Rock ni mtoto wa kwanza. Wazazi wake walikuwa na watoto saba, wavulana sita na msichana mmoja. Wadogo zake watatu Tony, Kenny na Jordan pia wako kwenye biashara ya burudani. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na saba Chris Rock aliacha shule. Baada ya kuacha shule alianza kufanya kazi katika vilabu vidogo vya uchekeshaji. Alipofanya kazi katika vilabu, Rock aligunduliwa na Mchekeshaji mwingine maarufu, Eddie Murphy. Rock aliigiza katika filamu za Eddie Murphy kama vile "Beverly Hills Cop II" na "I'm Gonna Git You Sucka".

Kazi hariri

Kazi ya Chris Rock ilianza kufanya vizuri alipoajiriwa kuwa kwenye " Saturday Night Live(SNL) ". Alifanya kazi kwenye SNL kwa miaka mitatu kwanzia 1990 hadi 1993. Aliondoka baada ya miaka mitatu na kuanza kufanya kazi kwenye tamthilia "In Living Color". Tamthilia zilianza mwezi mmoja baada ya Chris Rock kujiunga. Chris Rock baadaye alitengeneza tamthilia yake ya kwanza ya uchekeshaji iliyoitwa "Big Ass Jokes". Alitengeneza tamthilia hiyo mnamo 1994 na ilishinda Tuzo ya CableACE. Alitengeneza tamthilia yake ya pili ya uchekeshaji iliyoitwa “Bring the Pain”. Aliumba tamthilia hio mnamo mwaka 1996 na ilishinda tuzo mbili za Emmy. Mnamo mwaka 1999 na 2004 Chris Rock aliumba tamthilia nyingine mbili za uchekeshaji zilizoitwa " Bigger & Blacker " na " Never Scared ". Baada ya hapo alizingatiwa "mtu mcheshi zaidi Amerika". Aliumba tamthilia yake ya kwanza ya mazungumzo inayoitwa "The Chris Rock Show". Kazi yake ya televisheni ilimshindia jumla ya Tuzo tatu za Emmy na uteuzi 15. Kazi yake yenye mafanikio zaidi iliitwa "Everybody Hates Chris". Tamthilia inatokana na maisha ya Chris Rock wakati alipokuwa mtoto. Tamthilia yake iliteuliwa kwa Tuza ya Golden Globe mnamo mwaka 2006 kwa mfululizo Bora wa TV. Mnamo mwaka 2006 alishinda "Tuzo ya Peoples Choice" kwa vichekesho vinavyopendwa vya Televisheni na tuzo mbili za Emmy.

Maelezo mengine hariri

  • Chris Rock aliwahi kushikilia rekodi ya dunia kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi wakati wa tamthilia la vichekesho alipotumbuiza mbele ya watu 15,900 huko London mnamo mwezi wa tano mwaka la 2008.
  • Chris Rock hakujifunza kuogelea hadi alipokuwa na umri wa miaka hamsini na tano Sasa anaishi katika jimbo la New Jersey mji wa Alpine

Tanbihi hariri

  1. "Chris Rock | Biography, Movies, TV Shows, & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-26. 

Viungo vya nje hariri