Kidudu mtu

(Elekezwa kutoka Spalgis)
Kidudu mtu
Mabundo ya Spalgis epius.
Mabundo ya Spalgis epius.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Nondo na Vipepeo)
Nusuoda: Glossata (Vipepeo wenye ulimi mrefu)
Familia ya juu: Papilionoidea
Familia: Lycaenidae
Nusufamilia: Miletinae
Jenasi: Spalgis
Moore, 1879
Ngazi za chini

Spishi 7, 2 katika Afrika ya Mashariki :

Kidudu mtu (kwa Kiingereza: African apefly) ni jina linalotumiwa kwa ajili ya kutaja bundo la vipepeo wa jenasi Spalgis. Bundo hilo lina umbo ambalo linafanana kidogo na uso wa binadamu (au sokwe). Kama mabundo yote, linaendelea kubadilika mdudu kamili ambayo ni kipepeo.

Anapatikana sehemu kadhaa za Tanzania na nchi nyingi za Afrika. Hupendelea mazingira yenye majani mapana, hasa katika sehemu nyingi za ukanda wa ziwa Viktoria. Huzungukwa na poda nyeupe sehemu zote.

Katika wilaya ya Bukombe hutokea wakati wa kiangazi na kusababisha uvumi usio kweli kuwa yanaleta madhara kiafya kwa kusababisha mauti au vidonda kwenye mdomo pindi mboga hizo zinapotumika kwa chakula kwa hoja kwamba ana sumu kali[1].

Serikali ya wilaya hiyo imetangaza kuwa wadudu hao ni rafiki wa mkulima kwa sababu viwavi wao wanakula wadudu waharibifu wa vidung'ata (mealybugs) wanaoshambulia mazao mbalimbali kama vile mihogo, mipapai, mbaazi, nyanya, pamba na mipera[2].

Vipepeo hawa wana uhusiano na mbawabuluu, lakini viwavi wao hawaingii makoloni ya sisimizi. Hata hivyo, sisimizi hawawashambulii.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Spalgis jacksoni
  • Spalgis lemolea

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  • Takanami, Yusuke & Seki, Yasuo (2001). "Genus Spalgis". A Synonymic List of Lycaenidae from the Philippines. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 30, 2001. Iliwekwa mnamo 2022-12-18 – kutoka Internet Archive. {{cite web}}: More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) With images.