Stani
Stani (ing. tin) ni elementi. Namba atomia yake ni 50 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 118.710. Jina ni neno la kilatini stannum kwa metali hii.
Stani (stannum; kiing. tin) | |
---|---|
Vipande vya stani
| |
Jina la Elementi | Stani (stannum; kiing. tin) |
Alama | Sn |
Namba atomia | 50 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 118.710 |
Valensi | 2, 8, 18, 18, 4 |
Densiti | 7.31 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 505.08 K (231.93 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2875 K (2602 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 3 · 10-3 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo | Stani kwa mazingira ya wastani ina alotropi mbili au maumbo mawili yaani stani nyeupe na stani kijivu |
Ni metali laini sana yenye rangi ya kifedha-kijivu. Huyeyuka mapema kwenye kiwango cha halijoto cha 505 °C. Hupatikana hasa kama oksidi katika mitapo.
Matumizi ya kihistoria
haririKatika historia ilikuwa kati ya metali za kwanza zilizotumiwa na binadamu katika teknolojia. Bronzi ambayo ni aloi ya shaba na stani ilikuwa metali ya kwanza ya vifaa vya kazi na silaha katika nchi nyingi kabla ya teknolojia ya chuma. Mahitaji ya stani yalikuwa sababu muhimu kwa Waroma kuvamia Britania penye migodi muhimu ya stani katika rasi ya Cornwall.
Matumizi ya kisasa
haririMatumizi ya stani duniani ni takriban tani 300,000 kwa mwaka.
Theluthi moja ya mahitaji ni kwa ajili ya aloi za lihamu kwa kazi za kulehemia. Matumizi haya yamezidi kuwa muhimu kutokana mahitaji makubwa ya kompyuta na vifaa vya elektroniki.
Stani haioksidiki kirahisi hewani na hujiunga na chuma. Hivyo theluthi nyingine ya mahitaji ya stani ni kama koti kwa mabati ya chuma au kwa bati za kopo ni kinga dhidi ya kutu.