Stefano ni mfiadini wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo.

Stefano alivyochorwa na Giotto.

Habari zake zinapatikana katika kitabu cha Matendo ya Mitume kuanzia sura ya 6.

Myahudi mwenye kutumia zaidi lugha ya Kigiriki, ni kati ya wanaume 7 wa kwanza kuwekewa mikono na Mitume wa Yesu kwa ajili ya huduma.

Kutokana na juhudi zake, alikabiliana na chuki ya Wayahudi wenye msimamo mkali.

Kifodini chake kilitokea Yerusalemu labda mwaka 36 BK. Katika kufa alimuiga Yesu kwa kuwaombea msamaha watesi wake akamkabidhi roho yake. Maneno yake ya mwisho yalikuwa haya (Mdo 7:59-60): "Bwana Yesu, pokea roho yangu… Bwana, usiwahesabie dhambi hii."

Mhusika mkuu wa kifo chake alikuwa Farisayo jina lake Saulo, maarufu zaidi baadaye kwa jina la Mtume Paulo.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na madhehebu yote ya Ukristo yanayokubali hadhi hiyo.

Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu yake tarehe 26 Desemba[1], wakati Waorthodoksi wanafanya hivyo tarehe 3 Agosti.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stefano kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.