"Still D.R.E." ni wimbo wa Dr. Dre, umetolewa ukiwa kama wimbo kingozi wa albamu iliopata maplatinam kedekede ya 2001. Wimbo huu umemshirikisha msanii Snoop Dogg mwanzoni, kwenye kiitikio na mwishoni pia.

“Still D.R.E.”
“Still D.R.E.” cover
Single ya Dr. Dre
kutoka katika albamu ya 2001
B-side "Xxplosive"
Imetolewa Oktoba, 1999 (12")
9 Mei 2000 (Maxi)
Muundo CD5, 12"
Aina West Coast hip hop
Gangsta rap
Urefu 4:34
Studio Aftermath/Interscope
Mtunzi Melvin Bradford
Shawn Carter
Calvin Broadus
Scott Storch
Andre Young
Mtayarishaji Dr. Dre, Mel-Man na Scott Storch
Mwenendo wa single za Dr. Dre
"Fuck You
(1999)
"Still D.R.E."
(1999)

Historia

hariri

Wimbo huu ulikuwa maarufu sana, na ilisaidia albamu hii kufikia kiwango cha maplatinamu mengimengi. Mashairi yake, yaliandikwa pia na Jay-Z (alitumia jina la S. Carter katika maelezo ya vinoti vya albamu) na yanamtaja kuwa Dre amejea kwenye uwanja wa muziki wa hip hop kama kawa. Sampuli ya wimbo:

Kiingereza

Ladies, they pay homage, but haters say Dre fell off/How nigga? My last album was The Chronic.

Kiswahili

Mabibi, wanatoa heshima, lakini wenyechuki wanasema Dre ameanguka/Inakuwaje washikaji? Albmu yangu ya mwisho ilikuwa The Chronic.

Wimbo ulitayarishwa na Dre na Mel-Man, akiwa pamoja na Camara Kambon na Scott Storch kwenye vinanda, ambaye aliyetengeneza vinanda mashuhuri vya riff. Iliangia moja kwa moja katika chati za Billboard Hot 100 ikiwa katika nafasi ya 93, lakini haikuchukua muda kwenye chati hiyo ikaondoshwa.

Matayarisho

hariri
  • Mhandisi - Richard Huredia
  • Mhandisi Msaidizi - Jeff Burne , Michelle Forbes , Steve MacAuley
  • Vinanda - Scott Storch na Camara Kambon
  • Imewekwa sawa na - Brian Gardner
  • Imemixiwa na - Dr. Dre
  • Imetayarishwa na - Dr. Dre , Mel-Man
  • Washiriki wa Kurap - Snoop Dogg

Video yake

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri