Sudusi (kundinyota)
Sudusi (kwa Kilatini na Kiingereza Sextans) [1] ni jina la kundinyota dogo karibu na ikweta ya anga.
Mahali pake
haririSudusi iko kati ya makundinyota ya Asadi (Leo, pia Simba) na Shuja (Hydra) ikigusana pia na Batiya (Crater). Iko karibu na ikweta ya anga. Nyota angavu ya Maliki Junubi (ing. Regulus) iko jirani.
Jina
haririKundinyota hili haikujulikana kwa mabaharia Waswahili wa Kale wala kwa Waarabu au Wagiriki kwa sababu nyota zake ni hafifu na chache. Ni kati ya makundinyota yaliyoanzishwa na mwanaastronomia Johannes Hevelius, Mjerumani kutoka Danzig (wakati ule milki ya Poland), katika mwaka 1690 BK. Hevelius aliyeandika kwa Kilatini alichagua jina “Sextans” ambacho ni kifaa kilichotumiwa na mabaharia na wanaastronomia, pia na wanajimu kupima pembe la mahali pa nyota na umbali kati ya nyota, kwa mfano kwa kusudi la kukadiria nafasi yao baharini. Neno Sextans linamaanisha sehemu ya sita ya duara, yaani sudusi. Hevelius, akiwa mpika pombe na mfanyabiashara tajiri aliyeendelea kushika kwa muda uraisi wa mji wake, alikuwa hasa maarufu kwa kuangalia, kupima na kuorodhesha nyota pamoja na mke wake Elisabeth Hevelius.
Sextans - Sudusi ipo kati ya nakundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2] kwa jina la Sextans. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni 'Mic'.[3]
Nyota
haririSudusi –Sextans ina nyota chache na hafifu tu, Nyota angavu zaidi ni Alfa Sextantis yenye mag 4.49 ikiwa na umbali wa miaka nuru 280 kutoka Dunia[4]
Tanbihi
hariri- ↑ Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Sextans " katika lugha ya Kilatini ni "Sextantis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Sextantis, nk.
- ↑ The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
- ↑ Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy. 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R.
- ↑ Alpha Sex, tovuti ya Prof. Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Viungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sudusi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |