Uswahilini ni jina la nchi ya "Waswahili" yaani eneo kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki ambako lugha ya Kiswahili inatumiwa na desturi pia utamaduni vya watu vinaonyesha tabia jinsi zilivyo kawaida kati ya Waswahili .

Uswahilini ni makazi yanayokaliwa na Waswahili hasa wakizungumza lugha ya kiswahili ambayo imezaliwa hasa katika pwani ya Afrika mashariki na visiwa vilivyomo pembeni mwa pwani hiyo. Uswahilini ni makazi yaliyotapakaa hasa nchini Tanzania ambapo inamaanisha hasa msongamano wa nyumba za hali ya chini, tofauti na Uhindini na Uzunguni, mitaa inayokaliwa na Wahindi na Wazungu. Dar es Salaam ni moja ya miji iliyotapakaa na Uswahili ambapo wenyeji wenyewe husema ni Uswahili.