Susan B.Anthony

mwanaharakati wa haki za wanawake wa Marekani

Susan Brownell Anthony (15 Februari 1820 - 13 Machi 1906) alikuwa kiongozi wa kutetea haki za wanawake nchini Marekani.

Susan B. Anthony

Susan B Anthony ca. 1900
Amezaliwa Susan Brownell Anthony
Februari 15, 1820

Katika umri wa miaka 17 alikuwa mwalimu wa shule, lakini muda mfupi baadaye alijihusisha na mambo ya utumwa na unywaji pombe.

Mnamo miaka ya 1850, alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Elizabeth Cady Stanton[1] kwa ajili ya kutetea haki za wanawake, ikiwemo haki ya wanawake kupiga kura.

Kwa miaka kadhaa alikuwa mhariri wa gazeti lililoitwa The Revolution. Mnamo mwaka 1872 alikamatwa kwa kosa la kujaribu kupiga kura.

Kwa miaka mingi, alikuwa kiongozi wa chama cha kitaifa cha kutetea haki ya upigaji kura kwa wanawake kilichoitwa National Women's Suffrage Association, ambacho kilijikita katika kuhakikisha wanawake wanapata haki ya kupiga kura nchini Marekani kwa kipindi hicho.

Mnamo mwaka 1920 mabadiliko ya 19 ya katiba ya Marekani yalipitishwa, ambapo ilikuwa ni miaka 14 tokea kifo cha Susan B. Anthony kilichotokea 13 Machi 1906.

Susan B. Anthony alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa kwenye sarafu ya Marekani, dola.[2]

References

hariri
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-30. Iliwekwa mnamo 2017-07-15.
  2. https://en.wikipedia.org/wiki/Susan_B._Anthony_dollar

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Susan B.Anthony kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.