Swahili Rap from Tanzania


Swahili Rap from Tanzania ni jina la albamu ya nyimbo mchanganyiko za muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Albamu imetoka tarehe 15 Novemba mwaka wa 2004 chini ya kampuni ya Kijerumani maarufu kama Out Here Records. Albamu imetayarishwa na studio mbalimbali jijini za jijini Dar es Salaam. Albamu ina nyimbo kali kibao za miaka ya 2003 na 2004 yenyewe. Nyimbo hizo kama vile Zali la Mentali, Wauguzi, Alikufa kwa Ngoma, Asali wa Moyo na nyingine kibao.[1][2] Hii ndiyo albamu ya kwanza ya nyimbo mchanganyiko za Bongo Flava kupata kutumiwa na mashirika ya kimataifa.

Swahili Rap From Tanzania
Swahili Rap From Tanzania Cover
Compilation album ya Wasanii Mbalimbali
Imetolewa 15 Novemba, 2004
Imerekodiwa 2002-2003-2004
Aina Bongo Flava, Hip hop
Urefu 70
Lebo Out Here Records
Mtayarishaji Mbalimbali

Orodha ya nyimbo

hariri
  1. Umoja Wa Tanzania - Juma Nature akiwa na Professor Jay
  2. Wauguzi - Wauguzi - Wagosi wa Kaya wakiwa na The First Mack
  3. Alikufa Kwa Ngoma - Mwana FA akiwa na Lady Jay Dee
  4. Zali La Mentali - Professor Jay akiwa na Juma Nature na Muny
  5. Usinichanganye Mi - LWP Majitu
  6. Asali Wa Moyo - Gangwe Mobb
  7. Ama Zangu Ama Zao - GK akiwa na Lady JD na East Coast Team
  8. Maji Ya Shingo - Daz Nundaz
  9. Mtazamo - Afande Sele akiwa na Solo Thang na Professor Jay
  10. Mkiwa - K-Sal akiwa na Feruzi
  11. Anakuja - Sista P
  12. Mi Mmasai Remix - Mr. Ebbo
  13. Dunia Dudumizi - X-Plastaz

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Swahili Rap from Tanzania katika wavuti ya Discogs
  2. Swahili Rap from Tanzania katika wavuti rasmi ya Out Here Records.