Pange

familia ya wadudu
(Elekezwa kutoka Tabanidae)
Pange
Dume la pange madoa-mawili (Tabanus biguttatus)
Dume la pange madoa-mawili (Tabanus biguttatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Familia ya juu: Tabanoidea
Familia: Tabanidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 3:

Pange ni nzi wa familia Tabanidae katika oda Diptera ambao wanafyonza damu ya mamalia pamoja na watu. Wanaweza kuenezea watu na wanyama vidusia kama vijidudu au minyoo. K.m. spishi za jenasi Chrysops hupisha minyoo kama Loa loa na Loa papionis, ambao huishi chini ya ngozi.

Nzi hawa huwa na ukubwa wa nzi-nyumbani au zaidi, hadi mm 25. Mwili ni mpana na macho makubwa. Sehemu za kinywa ni vijembe sita katika kunjo la labio. Vijembe hivi, vinavyoweza kuwa na meno kwenye makali, hutumika kwa kukata ngozi na vena ili kufikia damu.

Chakula cha pange ni mbochi na kiowevu au utomvi unaorishaiwa na mimea. Spishi nyingi ni wachavushaji muhimu wa maua. Ijapokuwa madume na majike hula mbochi, majike wanahitaji chakula chenye kiwango cha juu cha protini na kwa hivyo hufyonza damu ya mamalia. Kwa kawaida huchagua wanyama wakubwa, kama vile farasi, ngamia, kulungu na ng'ombe, lakini spishi nyingine zimeonwa kufyonza damu ya mamalia wadogo, ndege, mijusi na makobe.

Kuumwa na pange kunaleta uchungu. Kwa kawaida, kirugu (sehemu ya ngozi iliyonyanyuka) hufanyika kilichozunguka mahali pa kuumwa, na dalili nyingine zinaweza kuwa pamoja na urticaria (ukurutu), kizunguzungu, udhaifu, kukoroma, na angioedema (kidonge pinki au chekundu kwa muda kwenye midomo au kuzunguka macho). Watu wachache hupata athari ya mzio.

Wakiuma pange wanaweza kupitisha vidusia: hujulikana kuwa vekta wa magonjwa ya mamalia yanayosababishwa na bakteria, virusi, protozoa na minyoo, kama vile virusi ya anemia ya kuambukiza ya farasi na spishi mbalimbali za Trypanosoma ambazo husababisha magonjwa katika wanyama na watu (k.m. nagana na ugonjwa wa malale). Spishi za jenasi Chrysops hupitisha minyoo vidusia aina za filaria Loa loa baina ya watu na Loa papionis baina ya nyani, na spishi nyingine hupitisha kimeta baina ya ng'ombe na kondoo na tularemia kati ya sungura na watu.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

hariri