Tafsiri ya Vishazi vya Kiingereza kwa Kiswahili

Vishazi ni vifungu vya maneno, aghalabu visivyo na kitenzi kikuu, ambavyo makala hii inafanya kazi ya kupatanisha vile vya Kiingereza na tafsiri ya Kiswahili katika mahusiano mema kati ya lugha na lugha. Sehemu ya kwanza ya maelezo inatoa ufafanuzi wa maana. Sehemu ya pili ya maelezo inaelekeza jinsi ya kusema (kisawe) kwa ufupi.

Maudhui hariri

Kishazi cha Kiingereza, declare interest kina maana ya kuweka wazi, kubainisha au kuwaambia wakusikilizao/uwaandikiao kuhusu maslahi yako binafsi juu ya jambo au kitu au mada unayozungumzia. Katika kusema kwa ufupi, tamka: nabainisha maslahi binafsi au naweka wazi maslahi binafsi au nawajulisha kuwa nina maslahi binafsi katika hili, na kadhalika.

Bad luck ni kishazi chenye maana ya kinahau. Huelezea kutokea kwa jambo lenye athari mbaya bila kutarajiwa au kudhamiriwa. Kisawe chake ni bahati mbaya.

It is unlucky/unfortunate ni kishazi kinachoelezea kutokea kwa jambo isivyotarajiwa au si la kupendeza au baya na la kushitukiza. Kisawe cha Kiswahili ni si bahati, haikuwa bahati.

Download a file ni mchakato wa kuchukua nakala ya faili (maandishi, taswira, video, n.k.) kutoka sehemu fulani mtandaoni, kuiingiza na kuihifadhi kwenye kifaa chako (simu, kishikwambi, kompyuta, n.k.). Kishazi kisawe: pakua faili.

Upload a file ni mchakato wa kuliingiza faili la kielekroniki (maandishi, taswira, video, n.k.) kwenye sehemu iliyodhamiriwa mtandaoni. Kishazi kisawe chake cha Kiswahili ni pakia faili.

Critical thinking ni kufikiri kwa kina kunakoambatana na tafakuri, kujiuliza maswali na kuyatafutia majibu. Pia huhusisha ukosoaji ama kuunga mkono dhana mbalimbali baada ya kujiridhisha. Kisawe chake kwa Kiswahili ni fikra tunduizi.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tafsiri ya Vishazi vya Kiingereza kwa Kiswahili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.