Taizé
Jumuia ya Taizé (kwa Kifaransa La communauté de Taizé) ipo kusini mwa mkoa wa Burgundy, Ufaransa. Ndipo nyumba kuu ya jumuiya hiyo ya kimataifa ilipoundwa rasmi na Bruda Roger Schutz (1915-2005) mwaka 1940. Baada ya mwanzilishi kuuawa na kichaa. kiongozi wa jumuia ni Bruda Alois.
Karama
haririMabruda wanajitolea maisha yao kushirikiana katika mambo ya kiroho na mali (vitu), kuishi kwa useja, ufukara/maisha ya hali ya chini.
Kwa sasa wapo mabruda zaidi ya 100 wanaotoka katika nchi ishirini na tano; wengi wao ni waamini wa Kanisa Katoliki na madhehebu mbalimbali yenye chimbuko la Kiprotestanti ambao wana juhudi za pekee kwa ajili ya ekumeni.
Utume
haririTangu mwishoni mwa miaka ya 1950 mamilioni ya vijana wenye umri wa utu uzima toka nchi mbali mbali wamefika Taizé kushiriki mikutano ya sala na tafakuri za kila juma.
Pia mabruda wa Taizé hutembelea na kuongoza mikutano/kongamano ya aina mbalimbali, mikubwa na midogo, katika mabara yote ya dunia ikiwa ni aina ya hija inayolenga kujenga misingi ya kuaminiana.
Ratiba ya jumuia
haririKutoka jumatatu hadi ijumaa
8.15 am sala za asubuhi, zikifuatiwa na kifungua kinywa 10.00 am bruda huanzisha somo la siku likifuatiwa na tafakuri ya kimya au ya majadiliano katika makundi madogomadogo 12.20 pm sala ya katikati ya siku, ikifuatiwa na mlo cha mchana 2.00 pm mazoezi ya kuimba kwa wanaopenda 3.30 pm kazi za mikono/ makundi madogo madogo ya kimataifa 5.15 pm chai 5.45 pm warsha kuanzia jumanne 7.00 pm mlo wa usiku 8.30 pm sala za usiku, zikifuatiwa na mkesha pamoja na nyimbo kanisani, na kufuatiwa na kimya
Ijumaa: sala za jioni hufuatiwa na sala kuuzunguka msalaba. Jumamosi: sala za jioni pamoja kuwasha mishumaa kusheherekea fumbo la pasaka. Jumapili:
8.45 am kifungua kinywa 10.00 am ibada ya misa ya asubuhi 1.00 pm mlo wa mchana 7.00 pm mlo wa usiku 8.30 pm sala ya jioni