Tafakuri (kutoka neno la Kiarabu linalokazia kufikiri) ni zoezi la binadamu katika kutumia vema akili yake.

Sanamu ya Buddha akiwa anatafakari.
Watu wakitafakari huko Madison Square Park, New York City, Marekani.
Akiamini sana tafakuri katika Ukristo, Mtakatifu Pio wa Pietrelcina alisema: "Kwa kusoma vitabu, mtu anamtafuta Mungu; kwa kutafakari mtu anampata".[1]

Lengo linaweza kuwa utulivu wa nafsi, ambao unasaidia pia afya ya mwili, au uchimbaji wa jambo fulani, au utafutaji wa jibu la swali lililojitokeza, au uamuzi kuhusu maisha au mengineyo ya namna hiyo.

Tafakuri za makusudi lilitumika toka zamani katika dini mbalimbali hata kwa kufumba macho, kukariri maneno fulani, kutumia tasbihi za aina mbalimbali, n.k.

Kwa namna ya pekee, tafakuri inazingatiwa katika monasteri.

Tanbihi hariri

  1. The Rosary: A Path Into Prayer by Liz Kelly 2004 ISBN 0-8294-2024-X pages 79 and 86

Marejeo hariri

Marejeo mengine hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.