Tel Aviv-Yafa (kwa Kiebrania תֵּל־אָבִיב-יָפו; kwa Kiarabu تَلْ أَبِيبْ-يَافَا) ni mji mkubwa wa pili nchini Israel, wenye wakazi 460,613 (2019)[1]. Rundiko la mji kuna watu zaidi ya milioni 3. Mji uko kando ya bahari ya Mediteranea.

Uso wa Tel Aviv-Yafa upande wa pwani

Historia

hariri

Mji ulitokana na maungano ya miji ya Yafa na Tel Aviv mwaka 1949 baada ya vita ya Kiarabu-Kisraeli ya 1948. Wakati ule Tel Aviv ilikuwa mji mkubwa na Yafa ilibaki na watu wachache tu baada ya kukimbia kwa wakazi Waarabu wengi vitani.

Tel Aviv ilianzishwa kando ya mji wa kale wa Yafa mwaka 1909 na Wayahudi waliohamia Palestina kutoka Ulaya. Mwanzoni ilikuwa kitengo tu cha Yafa kilichojitawala lakini kiliendelea kukua haraka kushinda mji wa kale kikawa manisipaa mwaka 1934.

Wakati wa utawala wa Uingereza Tel Aviv ilikuwa kitovu cha maisha ya Kiyahudi katika Palestina. Hadi leo Tel Aviv-Yafa ni kitovu cha kiutamaduni na cha kiuchumi cha nchi ya Israel.

Marejeo

hariri
  1. "Population in the Localities 2019" (XLS). Israel Central Bureau of Statistics. Retrieved 16 August 2020.

Viungo vya nje

hariri