The Verteller

Albamu ya muziki, Dizasta Vina

"The Verteller" ni jina la albamu ya pili ya msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Dizasta Vina. Albamu ilitolewa rasmi mnamo tarehe 27 Desemba, 2020 chini ya lebo ya Panorama Authentik. [1] Albamu ina jumla ya nyimbo 20. Sehemu kubwa ya albamu imetayarishwa na Ringle Beatz (ambaye pia amesimama kama mtayarishaji mkuu), vilevile kuna watayarishaji wengine ambao wamechangia kwenye kutayarisha na kuchanganya muziki. Watayarishaji hao ni pamoja na Cjmoker na Jcob. Nyimbo zilizotolewa kama singo ni pamoja na Ndoano, Nobody Is Safe 3 na Wimbo usio bora.

The Verteller
Studio album ya Dizasta Vina
Imetolewa 27 Desemba, 2020
Imerekodiwa 2019 - 2020
Aina Hip hop, Bongo Flava
Urefu 100
Lebo Panorama Authentik
Mtayarishaji Ringle Beatz (Mtayarisha Mkuu)
Cjmoker
Jcob
Dizasta Vina
Wendo wa albamu za Dizasta Vina
Jesusta
(2018)
The Verteller
(2020)
Single za kutoka katika albamu ya The Verteller
  1. "Ndoano"
    Imetolewa: 06 Oktoba, 2019
  2. "Nobody Is Safe 3"
    Imetolewa: 05 Julai, 2020
  3. "Hatia IV"
    Imetolewa: 13 Desemba, 2020
  4. "Wimbo usio bora"
    Imetolewa: 13 Machi, 2021


Albamu imeshirikisha wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tk Nendezi (wimbo wa Almasi), Adam Shule Kongwe, Bokonya na Wakiafrika (wimbo wa Maabara), Nasra Sayeed (wimbo wa Hatia IV), na Dash ambaye ameshirikishwa katika nyimbo tatu (wimbo wa A confession of mad son, A confession of mad philosopher" na Mwanajua).[2]

Neno "verteller" lina maana ya ‘msimuliaji’ kutokea lugha ya Kiholanzi. Jina linasanifu maudhui kwani albamu imesheheni masimulizi ya matukio yanayotokea mahala anapotokea msimuliaji kwa maana ya mtaa, mkoa au nchi. Dizasta Vina anaeleza kuwa albamu inaonyesha taswira ya elimu, imani, tamaduni na mila za jamii yake na jinsi zilivyojenga mtazamo wake wa sasa.

Historia na Kurekodi hariri

Albamu ilikuwa kwenye maandalizi kwa muda mrefu. Kwenye mahojiano yake aliyofanya tarehe 28 Julai, 2022 na kipindi cha "XXL" cha Clouds FM, Dizasta alifunguka mengi mno kuhusu albamu hii. Alieleza harakati za kuiandaa na kwanini albamu ilianza kutolewa kwa kuuzwa mikononi kabla ya majukwaa ya kidijitali. Dizasta alifafanua ya kwamba kazi ya kuirekodi ilianza mapema mwaka wa 2018 na kuendelea hadi 2020. Ilitumia muda mrefu kuiandaa na moja ya sababu ni kwamba kulikuwa na wazo la pili kwenye kila hatua.[3] Katika mahojiano hayo, Dizasta alifunguka kuwa nyimbo nyingi zilizokuwa zimerekodiwa na midundo tofauti na ile inayosikika kwenye albamu. Muziki ulibadilishwa kila wazo jipya lilipokuja, yote ikilenga kuwa na muziki mzuri unaoendana na maudhui, hali na msisimko wa nyimbo husika. Albamu ilichukua karibia miezi 26, kuanzia kuandikwa hadi kuzalishwa na kusambazwa sokoni. [4]

Albamu inawakilisha wasifu wa msimuliaji na mahala anakotoka. Asilimia kubwa ya nyimbo za kwenye albamu hii ni hadithi ambazo visa vyake zimebuniwa lakini vinatoa picha ya maisha ya watu wa jamii yake. Albamu ina nyimbo 20 zinazo ongelea elimu, tamaduni, mitazamo, mila, imani ya vikundi mbalimbali vya watu wa jamii aliyotokea na hadithi nyingine zinazogusa nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu.[5] Dizasta alidai kuwa alisikiliza mara kwa mara albamu ya Mi Mmasai ya Mr Ebo na Machozi, jasho na damu ya Professor Jay wakati wa kuandaa albamu hii.

Nyimbo hariri

Wimbo wa kwanza kutoka kwenye albamu unaoitwa "Ndoano" ulitolewa tarehe 06 Oktoba 2019, na kufuatiwa na wimbo wa "Nobody is Safe 3" iliyotolewa tarehe 05 Julai 2020 na "The Verteller (intro)" iliyotolewa tarehe 27 Septemba 2020[6]. Wimbo wa kumi na tatu wa albamu "Wimbo usio bora" ulitolewa tarehe 13 Machi 2020. Video ya wimbo huu ambayo iliongozwa na Black X na kutayarishwa na Panorama Authentik, ilitolewa kwenye akaunti ya YouTube ya Dizasta Vina mnamo 13 Machi 2020.[7]

Mnamo tarehe 18 Februari 2022 Dizasta alitoa wimbo wa "A Confession of a Mad son" ambao ni wimbo wa saba kwenye albamu hii.

Orodha ya nyimbo hariri

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu ya "The Verteller".[8]

Na. Jina la wimbo Mtunzi Mtayarishaji Maelezo Urefu
1 The Verteller (Intro) Dizasta Vina Ringle Beatz 5:29
2 Kibabu Na Binti Dizasta Vina Ringle Beatz 4:59
3 Tatoo Ya Asili Dizasta Vina Dizasta Vina, Ringle Beatz 4:27
4 A Confession of a Mad Man Dizasta Vina Ringle Beatz 4:03
5 A Confession of a Mad Philosopher Dizasta Vina Ringle Beatz Kamshirikisha Dash 4:19
6 A Confession of a Mad Teacher Dizasta Vina Ringle Beatz, Dizasta Vina 4:11
7 A Confession of a Mad Son Dizasta Vina Ringle Beatz, Dizasta Vina Kamshirikisha Dash 4:59
8 Muscular Feminist Dizasta Vina Ringle Beatz 9:06
9 Mwanajua Dizasta Vina Ringle Beatz Kamshirikisha Dash 4:42
10 Hatia IV Dizasta Vina Ringle Beatz Kamshirikisha Nasra Sayeed 7:13
11 Ndoano Dizasta Vina Dizasta Vina, Ringle Beatz, Jcob 3:45
12 Money Dizasta Vina Ringle Beatz 5:11
13 Wimbo Usio Bora Dizasta Vina Ringle Beatz 5:14
14 Maabara Dizasta Vina, Bokonya, Adam ShuleKongwe, Wakiafrika Dizasta Vina,

Ringle Beatz

Kamshirikisha Bokonya, Wakiafrika na Adam Shulekongwe 6:47
15 Nobody Is Safe 3 Dizasta Vina Ringle Beatz 5:36
16 Yule Yule Dizasta Vina Ringle Beatz 3:57
17 Almasi Dizasta Vina, TK Nendeze Ringle Beatz Kamshirikisha TK Nendeze 4:39
18 Mlemavu Dizasta Vina Ringle Beatz 4:28
19 Kesho Dizasta Vina Ringle Beatz 3:35
20 Kifo Dizasta Vina Ringle Beatz, Dizasta Vina 4:16

Historia ya kutolewa hariri

Tarehe na miundo ya kutolewa kwa The Verteller
Eneo Tarehe Lebo Muundo Kumb.
Tanzania December 27, 2020 Diski Gandamize (CD)
Sehemu Mbalimbali June 2, 2021
  • Upakuaji wa dijiti
  • Streaming

Marejeo hariri

  1. The Verteller katika wavuti ya Audiomack.
  2. Dizasta Vina - The Verteller (in English), retrieved 2023-03-21 
  3. LIVE: XTRA VINA | NI STORY MOB + VINA | DIZASTA VINA ON XXL (in sw-TZ), retrieved 2022-08-04 
  4. Bernard Mwakililo (2022-05-27). Dizasta Vina - Simulizi, Ubunifu na Maisha ya Jamii yake Ndani ya Album ya The Verteller. (en). Medium. Iliwekwa mnamo 2022-05-29.
  5. Dizasta Vina: “The Verteller” | Micshariki Africa (sw). Iliwekwa mnamo 2022-05-29.
  6. TRANSSION: LHX. Ndoano - Dizasta Vina | Boomplay Music (en). Boomplay Music - WebPlayer. Iliwekwa mnamo 2022-05-29.
  7. Dizasta Vina - Wimbo usio bora (Official Music Video) (in sw-TZ), retrieved 2022-05-29 
  8. The Verteller by Dizasta Vina (in en-US), 2021-06-02, retrieved 2022-08-04