Nge-mjeledi
Nge-mjeledi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nge-mjeledi (Mastigoproctus giganteus) akionyesha pedipalpi na mjeledi
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Familia 1 na nusufamilia 4: |
Nge-mjeledi (kutoka Kiingereza whip scorpion) ni arithropodi wa oda Thelyphonida katika ngeli Arachnida wafananao na nge wa kawaida. Kama hawa wana miguu minane na pedipalpi zenye gando. Mjeledi wa jina lao ni aina ya mkia mrefu na mwembamba. Kama kawaida mwili wao una sehemu mbili: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio zilizoungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija. Nge-mjeledi wana macho manane, mawili mbele ya kefalotoraksi na matatu kwa kila upande wa kichwa. Pedipalpi zao zinafanana na zile za nge, lakini zina mwiba nyuma ya gando na maneno magumu kwa kitako chao ambayo hutumika kwa kukamua mawindo. Miguu sita tu hutumika kwa kutembea. Jozi ya kwanza imekuwa mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio.
Nge-mjeledi hawana sumu lakini wana matezi yanayotoa mchanganyiko wa asidi ya asetiki na asidi ya kapriliki wakisumbuliwa. Hula arithropodi wengine, pengine nyungunyungu na makonokono uchi pia.
Katika Afrika kuna spishi moja tu, Etienneus africanus, inayotokea Afrika ya Magharibi.
Picha
hariri-
Mastigoproctus baracoensis
-
Mastigoproctus colombianus
-
Typopeltis sp.