Theodor Curtius
Geheimrat Julius Theodor Curtius (27 Mei 1857 - 8 Februari 1928) alikuwa profesa wa Kemia wa Ujerumani katika Chuo Kikuu cha Heidelberg. Yeye ndiye aliyegundua kampaundi nyingi za diazo, hydrazini (H2N.NH2) na asidi hidrazoiki (HN3).
Alisoma kemia na mwenzie Robert Bunsen katika Chuo Kikuu cha Heidelberg na Hermann Kolbe katika Chuo Kikuu cha Leipzig, alipata udaktari wake mwaka 1882 huko Leipzig.
Baadaye alifanya kazi kutoka mwaka 1884 hadi 1886 na Adolf von Baeyer katika Chuo Kikuu cha Munich, Curtius akiwa mkurugenzi wa idara ya kemia ya uchambuzi katika Chuo hicho hadi 1889.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Theodor Curtius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |