Thomas Robert Malthus

Mch. Thomas Robert Malthus FRS (13 Februari 1766 - 23 Desemba 1834) [1] alikuwa mchungaji wa Kianglikana na mtaalamu wa uchumi aliyetunga nadharia maarufu kuhusu demografia, hasa uhusiano kati ya ongezeko la watu na kiasi cha bidhaa zinazopatikana.

Thomas Robert Malthus

Maoni juu ya demografia hariri

 
Insha juu ya kanuni ya idadi ya watu, 1826.

Malthus ni maarufu kwa nadharia zake juu ya idadi ya watu: kuongezeka kwake au kupungua kwa kujibu mambo anuwai. Alieleza nadharia zake katika insha yake "Essay on the Principle of Population" (Insha kuhusu Usuli za idadi ya Watu), iliyochapishwa mwaka 1798 na kupata matoleo mapya hadi 1826. Alidai kuwa kila ongezeko la idadi ya watu litakutana baada ya muda fulani na njaa, magonjwa na kuongezeka kwa kiwango cha vifo.

"Nguvu ya ongezeko la watu (power of population) inazidi nguvu iliyoko katika ardhi kuzalisha riziki kwa mwanadamu". [2] p13

Akiwa mchungaji wa Kianglikana, Malthus aliona hali hiyo kama mapenzi ya Mungu. p104-105 Kuamini kwamba mtu hangeweza kubadilisha maumbile ya mwanadamu, Malthus aliandika kwamba yeyote anayeangalia historia ya binadamu wakati wowote na mahali popote duniani atapaswa kukubali kwamba

  • ongezeko la idadi ya watu lina mpaka wake katika riziki zinazopatikana,
  • idadi ya watu huongezeka kila wakati njia za kujikimu zinaongezeka,
  • nguvu ya ongezeko la idadi ya watu hukandamizwa na taabu na uovu, na hivyo idadi halisi ya watu inabaki jinsi ilivyo". [2] p61

Hoja zake zikaja kufuatwa na wengi, lakini pia kupingwa kwa nguvu kutokana na kasi ya maendeleo na uzalishaji.

Marejeo hariri

  1. Several sources give Malthus's date of death as 29 December 1834. See Meyers Konversationslexikon (Leipzig, 4th edition, 1885-1892), "Biography" Archived 18 Mei 2013 at the Wayback Machine. by Nigel Malthus. But the 1911 Britannica gives 23 December 1834.
  2. 2.0 2.1 Malthus T.R. 1798. An essay on the principle of population. Oxford World's Classics reprint.
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thomas Robert Malthus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.