Thugz Mansion
"Thugz Mansion" ni wimbo ulioimbwa na msanii wa muziki wa hip hop 2Pac. Wimbo ulitolewa baada ya kufa kwake ikiwa na matoleo mawili mashuhuri yaliyotolewa kutoka katika albamu ya mwaka wa 2002, Better Dayz. Toleo la awali ili-rapiwa ikiwa na magitaa mawili ya akustika. Toleo lingine la akustika limemshirikisha rapa mwenzi-wake Nas na vilevile mwimbaji J. Phoenix. Ni wa pili kutoka katika wimbo wa mwisho wa kwenye Diski 1 ya Better Dayz. Toleo la remixi la "7", limemshirikisha mwimbaji Anthony Hamilton, ikiwa imeingizwa ukiwa wimbo wa 2 kwenye diski ya Better Dayz, ni wimbo pekee kutoka katika albamu kuwa na muziki wa video. Wimbo umeshika nafasi ya #19 kwenye chati za Billboard Hot 100. Toleo halisi la akustika pia linapatikana kwenye albamu ya Nas God's Son ikiwa chini ya jina la "Thugz Mansion (N.Y.)", ikiwa na mstari wa pili ulioimbwa na Tupac ikiwa inabadilishana-badilishana hadi kufikia kwenye mstari kamili wa Nas.
“Thugz Mansion” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya 2Pac akishirikiana na Nas na J. Phoenix kutoka katika albamu ya Better Dayz na God's Son | |||||
Imetolewa | 17 Januari 2002 | ||||
Muundo | CD | ||||
Imerekodiwa | 2001 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 4:12 | ||||
Studio | Amaru | ||||
Mtunzi | Tupac Shakur | ||||
Mtayarishaji | 7 Aurelius na Kon Artis (7" Remix version) A. Pittboss Johnson, Aulsondro "Novelist" Hamilton, Claudio Cueni and Michael Herring (Acoustic Version) | ||||
Mwenendo wa single za 2Pac akishirikiana na Nas na J. Phoenix | |||||
|
Thugz Mansion ulikuwa mfano wa 2Pac akiwa mbinguni. Wimbo huu ni mmoja kati ya nyimbo za 2Pac alizojichunguza na kujielezea kinafsi mno. Ndani ya wimbo huu, anazungumzia namna atakavyokufa na kupumzika kwa amani. Yaani, ya kwamba hatimaye amepata furaha pale akiwa katika sehemu ambapo matatizo yake na maumivu yake yamefikia kikomo. Na akisisitiza kusema kwamba ataishia mahala pa amani baada ya kufa kwake; pia ametaja majina kadhaa ya Waafrika-Waamerika mashuhuri (watu hao ni pamoja na: Marvin Gaye, Billie Holliday, Jackie Wilson, Sam Cooke, Malcolm X, Miles Davis) na tukio la kisiasa la hivi karibuni (yaani, Latasha Harlins), ambao wote katika hao anaamini ya kwamba wapo mbinguni.
Orodha ya nyimbo
hariri- "Thugz Mansion" - 7" Remix (Explicit)
- "Thugz Mansion" - Nas Acoustic (Explicit)
- "F*ck Em All" (Explicit)
- "Thugz Mansion" - CD-ROM video
Makala 2000s song-related bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Makala hii kuhusu wimbo wa hip hop bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |