Hidekeli
Mto Hidekeli (pia: Tigris; Kiajemi: tigr, kar.: دجلة, dijla, kituruki/Kikurdi: dicle, Kiaramu: deqlath, Kiebrania: חידקל hidekel) ni mto wa Asia ya magharibi. Pamoja na Frati ni mto mkubwa wa Mesopotamia.
Chanzo | Milima ya Taurus katika Uturuki |
Mdomo | Ghuba ya Uajemi kwenye Shatt al Arab |
Nchi | Uturuki, Syria, Iraq |
Urefu | 1,900 km |
Kimo cha chanzo | ?? m |
Tawimito | Diyala, Zab, Al-Khabur |
Mkondo | 1500 m³/s (wastani) |
Eneo la beseni | 258,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Mosul, Tikrit, Baghdad |
Etimolojia
haririJina la Kiswahili lina asili yake katika Kiebrania cha Biblia kinachohifadhi jina la kale kabisa cha Kiakkadi linaloendelea pia katika maumbo la jina hili kwa Kiarabu, Kituruki, Kikurdi na Kiaramu.
Mwendo
haririHidekel ina chanzo chake katika milima ya Uturuki ya Mashariki. Kwa kilomita chache inapita eneo la Syria halafu inaingia katika Iraq. Baada ya kuvuka milima ya Kurdistan inapita mji wa Mossul na kuingia katika tambarare ya Mesopotamia. Inafika Baghdad na kuendelea katika Iraq ya kusini hadi kuungana na mto Frati katika Shatt al Arab ambayo ni mpaka kati ya Iraq na Uajemi. Mdomo uko katika pembe la Ghuba ya Uajemi.
Mito ya kando
haririMito ya kando muhimu ni:
- katika Uturuki: mto Batman
- katika Iraq: mto Zab
- katika Uajemi: mto Karun
Malambo
haririUturuki na pia Iraq zimejenga malambo mbalimbali hasa kwa kusudi la maji ya kumwagilia maeneo makavu. Wataalamu wanaona hatari ya kuhatarisha ekolojia ya mto kwa njia hii. Lakini mazingira ya sehemu kubwa ya mwendo wa mto ni kavu sana na mahitaji ya maji ni makubwa. Faida ya malambo imekuwa mwisho wa mafuriko yaliyotokea zamani hasa katika mwezi wa Aprili wakati wa kuyeyuka kwa theluji milimani.
Malambo katika Uturuki
hariri- lambo la Kralkızı
- lambo la Dicle
- lambo la Cizre
- lambo la Ilısu
- lambo la Garzan
- lambo la Kayser
- lambo la Silvan
Malambo katika Syria
haririSyria inapanga kujenga vituo vya kuvuta maji kutoka Hidekeli
Malambo katika Iraq
hariri- lambo la Mossoul
- lambo la Samara
- lambo la Kut
- lambo la Makhul