Tinde ni kata ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania, yenye msimbo wa posta 37210.

Kata ya Tinde ina vijiji vifuatavyo: Jomu, Nyambui, Kituli, Ngokolo, Buchama na Nhumbili.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 21,196 [1]. Kwa mujibu wa kitabu cha makadirio ya watu kilichotolewa na bunge mwaka 2016 idadi ya watu ilikuwa 18,264. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,978 waishio humo.[2]

Wakazi wengi wa Tinde ni wakulima, wakifuatiwa na wafanyakazi na wafanyabiashara.

Mazao yanayolimwa kwa wingi katika kata ya Tinde ni mahindi na mpunga. Mpunga ndio zao tegemezi ambalo linalimwa kwa ajili ya biashara na chakula vilevile.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Shinyanga vjijini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania  

Bukene | Didia | Ilola | Imesela | Iselamagazi | Itwangi | Lyabukande | Lyabusalu | Lyamidati | Masengwa | Mwakitolyo | Mwalukwa | Mwamala | Mwantini | Mwenge | Nsalala | Nyamalogo | Nyida | Pandagichiza | Puni | Salawe | Samuye | Solwa | Tinde | Usanda | Usule


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tinde kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.