Ugonjwa wa Klinefelter

Ugonjwa wa Klinefelter (kifupisho cha Kiingereza: KS) pia inajulikana kama 47,XXY au XXY, ni seti ya dalili zinazosababishwa na kromosomu X mbili au hata zaidi katika wanaume badala ya moja tu. Kipengele cha msingi ni utasa.

Mara nyingi dalili zinaweza kuwa ngumu kutambulika, na watu wengi hawajui kama wameathirika. Wakati mwingine dalili ni maarufu zaidi na zinaweza kuhusisha misuli kuwa dhaifu, urefu mkubwa wa mwili, uratibu na ufanisi mbaya wa mwili, nywele chache mwilini, viungo vya uzazi vidogovidogo, ukuaji wa matiti, na hamu ndogo ya ngono.

Mara nyingi ni wakati wa kubalehe kwamba dalili hizi zinaonekana. Akili na maarifa ni vya kawaida; hata hivyo, matatizo katika kusoma na kuongea ndiyo makuu. Dalili ni kali zaidi zikiwemo kromosomu tatu au zaidi za aina hiyo.

Ingawa hakuna tiba inayoweza kutatua tatizo hilo, kuna njia za kuwasaidia waliopatwa nalo.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa Klinefelter kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.