Ulaya ya Kusini
Ulaya ya Kusini ni sehemu ya kusini ya bara la Ulaya. Kuna maelezo ya kutofautiana ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hili. Maelezo hutofautiana kutokana na njia mbalimbali za kuangalia sehemu hiyo: kwa maana ya kijiografia, kisiasa au kiutamaduni.
Kwa hakika tamko hili lamaanisha:
- Nchi za rasi ya Iberia yaani Hispania, Ureno na Andorra.
- Nchi za rasi ya Italia yaani Italia, San Marino na Mji wa Vatikani
- Malta
- Ugiriki
Kwa kawaida nchi zifuatazo au sehemu zifuatazo za nchi huhesabiwa humo pia:
- sehemu za kusini za Ufaransa
- sehemu za Uturuki kwenye bara la Ulaya
- Kupri hata kama ni sehemu ya Asia kijiografia
Mara nyingi pia sehemu ya nchi za Balkani zahesabiwa humo:
Zote zinapakana na Mediteranea isipokuwa Masedonia Kaskazini.
Wakati mwingine Bulgaria huhesabiwa hapa pia.
Kanda la Umoja wa Mataifa
haririUmoja wa Mataifa huhesabu nchi zifuatazo kama nchi ya kanda la Ulaya ya Kusini: