Upendo Nkone ni mwimbaji wa kisasa nchini Tanzania. Anaimba nyimbo za Mungu na sauti kubwa sana na kwaya yake wanaweza vizuri kumsaidia.

Nkone alizaliwa sehemu ya Kigoma ingawa alipokuwa mtoto akahamia jijini Dar es Salaam ambapo akalelewa.

Sasa hivi, yeye ni mjane na ana watoto wawili. Nyimbo zake nyingi zinawaambia wajane, mayatima na wengine walio na matatizo kujipa moyo na kusonga mbele kwa furaha kwa sababu Mungu anawalinda. Ametunga nyimbo za kutosha kujaza albamu mbili na zote ni nzuri sana. Hasa nyimbo hizi ‘Usifurahi juu yangu’ na ‘Upendo wa Yesu’ zinapendwa sana na Watanzania. Ndiyo maana yeye ni shujaa wa muziki wa Injili wa sasa hizi.

Katika mwaka wa 2010 Upendo Nkone alitaja kuwa ataolewa tena. Vilevile, nyimbo mpya zinapatikana kama hizi: 'Usinipite bwana' na 'Zipo faida'.

Upendo Nkone anaimba nyimbo zinazohusu wokovu, hivyo ni jambo jema kutilia maanani jumbe zake.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upendo Nkone kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.