Urais wa Barack Obama

Urais wa Barack Obama ulianza tarehe 20 Januari 2009 saa sita mchana EST, alipoapishwa kama rais nambari 44 wa Marekani. Obama alikuwa mjumbe katika Bunge La Maseneta La Marekani kutoka Illinois alipomshinda mjumbe wa Arizona, Seneta John McCain, katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2008.

Sera zake Obama zimejumuisha majaribio ya kuyaondoa matatanisho ya kiuchumi ya miaka 2008-2009, na pia mabadiliko katika sheria za ushuru za Marekani. Katika sera zinazohusu nch za kigeni, Obama amejaribu kuukarabati uhusiano wa Mrekani na nchi nyingine, na pia kuanza kutamatisha ufungwaji wa mahabusu wa kigeni katika kituo cha kijeshi cha Guantanamo Bay. Obama ametanganza kwamba atajaribu kupunguza silaha za nyuklia zinazohifadhiwa na jeshi la Marekani.

Baraza la Mawaziri

hariri
Baraza la Mawaziri la Obama.
Wizara Afisi Waziri Picha Madarakani Tangu

Wizara ya Mambo ya Nje
Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Rodham Clinton 21 Januari 2009

Wizara ya Fedha
Waziri wa Fedha Timothy Geithner 26 Januari 2009

Wizara ya Kujihami
Waziri wa Kujihami Robert Gates 18 Desemba 2006

Wizara ya Sheria
Wakili Mkuu Eric Holder 2 Februari 2009

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri wa Mambo ya Ndani Ken Salazar 21 Januari 2009

Wizara ya Kilimo
Waziri wa Kilimo Tom Vilsack 21 Januari 2009

Wizara ya Biashara
Waziri wa Biashara Gary Locke 24 Machi 2009

Wizara ya Kazi
Waziri wa Kazi Hilda Solis 24 Februari 2009

Wizara ya Afya
Waziri wa Afya Kathleen Sebelius 28 Aprili 2009

Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji
Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miji Shaun Donovan 26 Januari 2009

Wizara ya Uchukuzi
Waziri wa Uchukuzi Ray LaHood 22 Januari 2009

Wizara ya Nishati
Waziri wa Nishati Steven Chu 21 Januari 2009

Wizara ya Elimu
Waziri wa Elimu Arne Duncan 21 Januari 2009

Waziri wa Mambo ya Wanajeshi Wastaafu
Waziri wa Mambo ya Wanajeshi Wastaafu Eric Shinseki 21 Januari 2009

Wizara ya Ulinzi wa Ndani na Usalama
Waziri wa Ulinzi wa Ndani na Usalama Janet Napolitano 21 Januari 2009

Viungo vya Nje

hariri