Useja mtakatifu ni aina ya useja ambayo mwanamume au mwanamke anaishika kwa hiari kwa sababu za kidini, hasa katika Ukristo, ambapo lengo ni kuungana zaidi na Yesu aliyeishi hivyo.

Lebo ya Useja mtakatifu ilivyochorwa na Giotto di Bondone, Firenze, Italia.
Toma wa Akwino, mwanateolojia bora za Karne za Kati, akivikwa na malaika mkanda wa usafi baada ya kuweka nadhiri ya useja mtakatifu.

Ndiye aliyehimiza wanaojaliwa kuelewa uhusiano wa useja na ufalme wa Mungu waushike kweli (Math 19:11-12).

Useja huo ni msingi wa aina zote za utawa na unadaiwa na Kanisa Katoliki kwa baadhi ya mashemasi na mapadri pamoja na maaskofu wote. Makanisa ya Kiorthodoksi yanaudai kwa maskofu tu.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.