Uwanja wa ndege wa Geita
Uwanja wa ndege wa Geita ni uwanja mdogo wa ndege wa kikanda kaskazini mwa Tanzania unaohudumia mji wa Geita. Uko karibu na mwambao wa kusini magharibi mwa Ziwa Viktoria takribani kilomita 14 (maili 8.7) kutoka mjini Chato. [1] Uwanja huu wa ndege una njia ndefu zaidi ya kurukia na kutua na ndio uwanja pekee wa lami katika Mkoa wa Geita.
Historia
haririUjenzi wa uwanja wa ndege ulianza mnamo 2017 Kilomita 14 (Maili 8.7) kusini mwa mji wa Chato na Kilomita 90 (Maili 56) magharibi mwa mji mkuu wa mkoa Geita. Mradi huo uligharimu TSh 40 bilioni na zilifadhiliwa kikamilifu na Serikali ya Tanzania. Uwanja huo wa ndege umejengwa kwa ajili ya kuhudumia mkoa wa Geita, mkoa unaozalisha zaidi ya nusu ya dhahabu zinazo uzwa nje ya nchi. [2]
Uwanja huo ulipata safari yake ya kwanza iliyopangwa Januari 2021 na Air Tanzania inayounganisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Mwanza . [3]
Rais Magufuli
haririUwanja huo wa ndege upo karibu na mji anakotoka rais wa 5 wa Tanzania John Magufuli. Katika safari mbalimbali za mkoa huo mwaka 2019 na siku za mwanzo za janga la COVID-19, pale ambapo Magufuli aliamua kusalia nyumbani, uwanja wa ndege ulikaribisha wakuu wa mikoa mbalimbali kwa ajili ya mikutano baina ya nchi mbalimbali. Hizi ni pamoja na
- Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya tarehe 5 Julai 2019 [4]
- Yoweri Museveni, Rais wa Uganda tarehe 13 Julai 2019 [5] na tarehe 13 Septemba 2020 [6]
- Filipe Nyusi, Rais wa Msumbiji tarehe 11 Januari 2021 [7]
- Sahle-Work Zewde, Rais wa Ethiopia tarehe 25 Januari 2021 [8]
Marejeo
hariri- ↑ "United Republic of Tanzania Govt Tender for Construction of New Chato Airport in Geita Region - 19". TendersOnTime (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ "Tanzania: Geita Airport to Receive Scheduled Flights Soon". allAfrica.com (kwa Kiingereza). 2020-12-14. Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ Shida, Yohana (2020-12-31). "Tanzania: Atcl Launches Direct Flights to Geita Airport". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ "President Uhuru Kenyatta arrives in Chato on a private visit". The East African (kwa Kiingereza). 2020-07-06. Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ "President Museveni meets Magufuli on 'pilgrimage' to Tanzania". State House of Uganda. 14 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Masare, Alawi (2020-09-14). "Tanzania: Magufuli, Museveni Give Green Light to $3.5 Billion Pipeline Project". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ mozambique. "Tanzania: Mozambique President Nyusi lays foundation stone for Chato hospital - Watch". Mozambique (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
- ↑ "Six issues dominate Tanzania, Ethiopia presidents' meeting in Chato". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-01-25. Iliwekwa mnamo 2021-11-26.
Makala hii kuhusu uwanja wa ndege nchini Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |