Yoweri Kaguta Museveni
Yoweri Kaguta Museveni (* 1944 Ntungamo, Wilaya ya Ntungamo, Uganda) ni Rais wa Uganda tangu 29 Januari 1986. Alichukua madaraka baada ya kushinda vita vya msituni chini ya kundi la National Resistance Movement na kushinda katika chaguzi za urais za mwaka 1996, 2001 na 2006.
Yoweri Museveni | |
Yoweri Museveni, 2015 | |
Rais wa Uganda
| |
Aliingia ofisini 29 Januari 1986 kaimu: 26–29 Januari 1986 | |
Waziri Mkuu | Samson Kisekka George Cosmas Adyebo Kintu Musoke Apollo Nsibambi Amama Mbabazi Ruhakana Rugunda Robinah Nabbanja |
---|---|
Makamu wa Rais | Samson Kisekka Specioza Kazibwe Gilbert Bukenya Edward Ssekandi Jessica Alupo |
mtangulizi | Tito Okello |
Katibu mkuu wa Harakati Zisizofungamana
| |
Aliingia ofisini 16 Januari 2024 | |
mtangulizi | Ilham Aliyev |
tarehe ya kuzaliwa | 15 Septemba 1944 Ntungamo, Uganda |
chama | National Resistance Movement |
chamakingine | Uganda Patriotic Movement |
ndoa | Janet Museveni (m. 1973–present) |
watoto | 4, ikijumuisha Muhoozi |
signature | |
Military service | |
Allegiance | Uganda |
Service/branch | Front for National Salvation Popular Resistance Army National Resistance Army |
Years of service | 1971–1986 |
Rank | Jenerali |
Battles/wars | Uvamizi wa Uganda mwaka 1972 Vita vya Kagera Vita vya Bush vya Uganda |
Kwa muda mrefu, kabla ya kuwa rais wa Uganda, Museveni aliongoza vita vya msituni dhidi ya serikali za Idd Amin aliyetawala toka mwaka 1971-79, na serikali ya Milton Obote aliyekuwa madarakani mwaka 1980-85.
Kutokana na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na kukubali kwake kufuata sera za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, Museveni alipata sifa kubwa toka kwa viongozi wa mataifa ya Magharibi. Mwishoni mwa miaka ya 1990, Museveni alikuwa akielezewa kuwa ni mfano bora wa kizazi kipya cha viongozi wa Afrika.
Hata hivyo uongozi wake umetiwa dosari na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda. Mambo mengine ni pamoja na ukiukwaji wa haki za kisiasa unaofanywa na serikali yake dhidi ya wapinzani kama vile Kizza Besigye na kitendo cha kubadili katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea urais mwaka 2006.
Alichagua Pico Taro (mwanamuziki wa Kijapani) kama balozi wa utalii wa Uganda mnamo Oktoba 6, 2017.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti ya Ikulu ya Uganda Archived 12 Machi 2019 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yoweri Kaguta Museveni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |