Mkoa wa Geita
Mkoa wa Geita ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Kagera upande wa magharibi, Shinyanga upande wa kusini na Mwanza upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Mkoa wa Geita |
|
Mahali pa Mikoa ya Geita na Mwanza katika Tanzania kabla ya umegaji | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | |
Mji mkuu | Geita |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa |
Makao makuu ya mkoa yapo Geita mjini.
Kabla ya kuanzishwa mkoa mpya wa Geita, eneo hili lilikuwa sehemu ya mkoa wa Mwanza ambao ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la km2 19,592. Mkoa wa Geita ulikadiriwa kuwa na wakazi 1,882,141 mnamo mwaka 2015.[1]
Wilaya za mkoa wa GeitaEdit
Wilaya za mkoa huo mpya ni
- Bukombe,
- Chato,
- Geita,
- Mbongwe na
- Nyang'hwale.
WakaziEdit
Makabila makubwa katika mkoa huu ni Wasukuma, Wasumbwa, Walongo na Wazinza.
Majimbo ya bungeEdit
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Geita Mjini : mbunge ni Costantine John Kanyansu (CCM)
- Geita Vijijini : mbunge ni Joseph Lwinza Kasheku ‘Msukuma’ (CCM)
- Busanda : mbunge ni Lolensia Bukwimba (CCM)
- Mbogwe : mbunge ni Augustino Masele (CCM)
- Bukombe : mbunge ni Doitto Mashaka Biteko (CCM)
- Chato : mbunge ni Dk. Medard Matogolo Kalemani (CCM)
Tazama piaEdit
TanbihiEdit
- ↑ 17 Population Distribution and Average Annual Intercensal Growth Rate by Region, Tanzania, Tanzania in Figures, tovuti ya Tanzania National Bureau of Statistics, iliangaliwa Septemba 2017
Viungo vya njeEdit
- Matokeo ya Sensa 2002 kwa Mwanza* Serikali ya TanzaniaArchived Desemba 15, 2003 at the Wayback Machine.
- Wasukuma Archived Julai 3, 2008 at the Wayback Machine.
- Geita investment profile Archived Machi 11, 2016 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |