Victoria Falls (mji)

Victoria Falls ni mji mdogo wa mkoa wa Matabeleland Kaskazini nchini Zimbabwe mwenye wakazi 35,199 (2022). Uko kando ya mto Zambezi mahali unapotelemka kwenye maporomoko ya Victoria Falls.

Maporomoko ya Victoria Falls pamoja na daraja kati ya Zimbabwe na Zambia.

"Vic Falls" jinsi inavyoitwa kwa kifupi ina mawasiliano kwa barabara na reli kwenda Hwangwe (km 109) na Bulawayo (km 440) upande wa kusini-mashariki. Mji wa karibu ni Livingstone katika Zambia ng'ambo ya mto. Daraja launganisha miji yote miwili.

Mji ulianzishwa mwaka 1901 ukastawi kama kituo cha reli karibu na maporomoko. Ulikuwa kitovu cha utalii kwenye maporomoko. Tangu mwaka 2000 utalii umerudi nyuma kutokana na matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Victoria Falls (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.