Vita vya kwanza vya Kiyahudi
Vita vya kwanza vya Kiyahudi dhidi ya Warumi (66–73 BK) vilifanyika hasa katika Yudea, sehemu ya Dola la Roma.
Vilifuatwa na vya pili (115–117), hasa nje ya Palestina (Libya, Misri, Kupro na Mesopotamia), na vya tatu (132–136), tena katika Yudea.
Pamoja na ushujaa wa Wayahudi waliopigania uhuru wa nchi yao, hatimaye Warumi waliteka na kuangamiza Yerusalemu na hekalu lake (70).
Habari hizo zilisimuliwa hasa na mwanahistoria Yosefu Flavius.
Tanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vita vya kwanza vya Kiyahudi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |