Kitambaa

(Elekezwa kutoka Vitambaa)

Kitambaa (pia kitambara) ni kipande cha tambaa au jora ambalo kimekatwa ili kushonea vazi la binadamu, kama vile shati, sketi au suruali, au kwa madhumuni mengine, kama vile kutandika meza, kochi au samani nyingine, kushonea pazia, kurembesha, kupenga, kuosha, kupangusa vitu zilizomwagikiwa kiowevu na pia vitu vikavu kama vile madirisha ya glasi n.k.

Kitambaa cha kitamaduni.

Siku hizi vitambaa vinatengenezwa kwa kawaida katika viwanda. Mara nyingi hutengenezwa kwa kuunganisha nyuzi pamoja, ziwe za asili au vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu. Mifano ya nyuzi za asili ni pamba na hariri. Mifano ya nyuzi zilizotengenezwa na binadamu ni nailoni na akriliki[1].

Rangi ya kitambaa inazingatiwa sana katika matumizi, kulingana na utamaduni, hali n.k.

Tanbihi Edit

  1. iLearnFashion (2018-01-25). Different Types of Fabrics Clothing Material Textile – Sources and Usages (en). Learn All About Fashion Outfits Beauty and Lifestyle. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-12-14. Iliwekwa mnamo 2018-12-20.

Marejeo Edit


  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitambaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.