Vitorini wa Ptuj (au wa Pettau; kwa Kilatini: Victorinus Petavionensis au Poetovionensis; karne ya 3 - Ptuj, leo nchini Slovenia, 303 hivi) alikuwa askofu wa mji huo hadi kifodini chake [1].

Mt. Vitorini katika mchoro wa ukutani huko Nova Cerkev (Slovenia).

Ingawa alimudu zaidi lugha ya Kigiriki, aliandika vitabu mbalimbali vya ufafanuzi wa Biblia ya Kikristo kwa Kilatini[2] , akiwa wa kwanza kufanya hivyo. Vingi vimepotea[3][4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[5] na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Novemba[6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.