Vivian (Paper Mario)
Vivian (kwa Kijapani: ビ ビ ア ン) ni mhusika wa kufikirika anayeonekana kwenye mchezo wa video wa mwaka 2004 kwa jina la Paper Mario: Mlango wa Miaka Elfu.[1] Hapo awali alikuwa kama adui wa mhusika Mario, baadaye kujiunga na mhusika huyu baada ya kumsaidia.[2] Katika toleo la Kijapani asili na katika tafsiri za ulaya. Vivian ni mwanamke wa jinsia tofauti na ile ya kuzaliwa. wakati katika matoleo ya Kiingereza ilibadilishwa na kumuonyesha kama ni mwanamke mwenye jinsia ya kuzaliwa nayo. Vivian ametajwa kuwa mmoja wa wahusika bora wa wapenzi wa jinsia moja kwenye michezo ya video. Kwa jinsi toleo la mchezo la Kijapani linavyomuonyesha na utambulisho wake wa kijinsia umepokea ukosoaji mkubwa sana.
Dhana na Utengenezaji
haririVivian ni mtu kama roho wa rangi ya zambarau, mwenye nywele nyekundu, glavu nyeupe, na kofia yenye rangi nyekundu na nyeupe mwenye uwezo wa kujificha kwenye vivuli na anaweza kudhibiti moto. Dada zake wawili wakubwa, Beldam na Marilyn, huvaa kofia za samawati na manjano mtawaliwa na hutofautiana kwa saizi.[3][4][5] Vivian ni mwanamke aliyebadilisha jinsia, na anadhihakiwa na Beldam, ambaye humdhihaki na kumwita mvaaji vitu na nguo ambavyo sio kawaida kuhusishwa na jinsia ya mtu husika.[3][4]
Wakati mchezo wa video wa Paper Mario: Mlango wa Miaka Elfu ulipotafsiriwa kwa Kiingereza na Kijerumani, Hadhi ya Vivian kama mwanamke aliyebadilisha jinsia ilibadilishwa na kuwa ya mwanamke mwenye jinsia asilia, na madhihaka kutoka kwa dada yake yalibadilishwa na kuonekana kuwa zilikuwa ni dhihaka juu ya sura yake.[3] Katika utafasiri wa mchezo ambao sio wa Kiingereza wala Kijerumani, Vivian bado anaonekana kuwa bado ni mwanamke aliyebadilisha jinsia.[6] Toleo la Kiitaliano, haswa, inasisitiza hadhi yake kama mwanamke aliyebadilisha jinsia kwa Vivian kuonyeshe kiburi kwa kubadili jinsia;[6] anajitapa dhidi ya uonevu wa dada yake kwa kusema "Ninajivunia kugeuka kuwa mwanamke!" [7]
Muonekano
haririVivian alionekana kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa video mnamo mwaka 2004 kwenye Paper Mario: Mlango wa Miaka Elfu.[3] Katika hadithi ya mchezo, yeye hapo awali alifanya kazi kama mshiriki wa Shadow Sirens, ambayo ni pamoja na dada zake wawili Beldam na Marilyn, wakifanya kazi dhidi ya Mario na washirika wake. Baadae Mario anamsaidia kutafuta kitu kilichokuwa kimepotea, bila kumtambua. Wakati anagundua aliyekuwa anamsaidia ni nani, Vivian mwanzoni anasita kumsaidia zaidi, lakini anaamua kujiunga naye kwa sababu ya dhihaka aliyopata kutoka kwa dada yake Beldam na wema ambao Mario alimwonyesha. Mwisho wa hadithi, Beldam anaapa kumheshimu.[8]
Anaonekana katika uigizaji tena kwenye mwendelezo, Super Paper Mario, wote kama kadi inayoweza kukusanywa na kama doli nzuri inayomilikiwa na mhusika. Anaonekana pia katika mkusanyiko wa Super Smash Bros. Brawl na Super Smash Bros Ultimate.[9]
Mapokezi
haririVivian amepokea mapokezi mazuri tangu aonekane katika mchezo wa video wa Mario: Mlango wa Miaka Elfu, na kuwa mhusika maarufu.[10] Mwandishi wa Nintendojo Mel Turnquist alijumuisha uamuzi wa Vivian wa kubakia upande Mario kama moja ya wakati wao wa kusisimua katika michezo ya video pia kwa sababu ya kuwa mdogo mwenyewe.[5] Sauti ya Uhuru iliita kasoro ya Vivian kutoka kwa dada zake kwenda kwa upande wa Mario inayoweza kuelezewa kwa watoto.[11] Kwingine ni pamoja na Vivian katika safu ambapo wanajadili uwezekano wa Super Smash Bros, wakielezea matumaini kwamba Vivian amejumuishwa badala ya chaguo la jadi kama vile Paper Mario[12]
Amepokea uangalizi wa juu sana hasa kwa hadhi yake ya mtu aliyebadilisha jinsia. IGN alimjumuisha Vivian katika orodha yao pendwa ya wahusika. Walimsifu Vivian kwa kutofafanuliwa na hadhi yake kama mtu aliyebadilisha jinsia, ingawa walionyesha kusikitishwa na kukasirishwa na mabadiliko kutoka kwa mwanamke aliebadilisha jinsia kwenda kwenye mwanamke mwenye jinsia asilia katika matoleo ya Kiingereza kwa sababu Vivian alikuwa mmoja wa wahusika wachache wenye hali hii katika michezo ya video.[6] Drag queen Daphne J. Sumtimez alimuorodhesha Vivian kama moja ya sanamu zake.[13]
Katika insha yao juu ya wahusika wa jinsia, waandishi Emil Christenson na Danielle Unéus wanajadili Vivian na jinsi jinsia ya Vivian ilivyoundwa.Wanataja mikono ya Vivian iliyoinama na kutabasamu mara kwa mara kama sifa za kike ambazo huonyesha kawaida. Pia wa rangi nyekundu ya kofia yake, wakigundua kuwa tofauti kati ya dada zake inaweza kuwa na nia ya kubadilisha jinsia yake. Wanakiri kupenda uhusika wa Vivian na wanakiri kuwa na mzuri, lakini unaonyeshwa vibaya kwa sababu ya dada zake kuwa wabaya.[14] Mwandishi Nicholas Taylor anamjumuisha katika sehemu ya wahusika wa jinsia ya kubadilisha kwenye kitabu Queerness in Play, akijadili jinsi jukumu la Vivian katika hadithi linaweza kusaidia wachezaji kuelewa uzoefu wao na jinsia, kitambulisho, na kujieleza.[15]
Hata hivyo wakosoaji wengine hawakufurahishwa na jinsi jinsia ya Vivian ilivyowasilishwa katika toleo la Kijapani. VG247 ilihisi kuwa kitambulisho cha jinsia ya Vivian kilionyeshwa kwa mtindo wa kiwazi.[16] Mwandishi Laura Kate Dale alikuwa akikosoa mazungumzo katika mchezo huo ambayo ilisema alikuwa wakati mmoja wa kiume, akihisi ilidokeza kuwa yeye hakuwa mwanamke wa kweli.[17] Katika uchambuzi wao kwa uwakilishi wa watu wanaobadilisha jinsia katika michezo ya video, waandishi Quincy Nolan na Ian Laih-Nolan walimjumuisha Vivian, vile vile wakikosoa lugha iliyotumiwa katika toleo la Kijapani kumuelezea lakini wakibainisha kuwa haiondoi "uwepo wake wa kupindua kijinsia;[18] Vivian amelinganishwa na mhusika mwenzake aliyebadilisha jinsia Nintendo Birdo, ambaye naye pia amebadilishwa jinsia katika michezo mingine na kubadilishwa utambulisho katika tafsiri ya Kiingereza.[17][3][4]
Marejeo
hariri- ↑ "Paper Mario". Super Mario Wiki (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Paper Mario: The Origami King Review". GameSpot (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Classic Nintendo Games That Were Censored | ScreenRant". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ 4.0 4.1 4.2 "Vivian in Paper Mario | LGBTQ Video Game Archive". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ 5.0 5.1 "Top Ten: Inspiring Moments « Nintendojo". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 "Our Favorite LGBTQ+ Characters In Games - IGN". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-08-10. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Paper Mario: The Thousand-Year Door - Mario Series Ending FAQ - GameCube - By Jelly Soup - GameFAQs". gamefaqs.gamespot.com. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Sticker List - Smash Bros. DOJO!!". www.smashbros.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-30. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ Tom Phillips (2020-07-17). "Paper Mario developer discusses why you don't see original characters like Vivian anymore". Eurogamer (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "6 Reasons Kids Should Play Paper Mario: The Thousand-Year Door - Guardian Liberty Voice". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "'Smash Bros. Ultimate' Roster Dreams: Vivian Adds 'Paper Mario' to the Game | Inverse". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Papermag's New Favorite Drag Queens Hit the Beach in a Super Swimsuit Extravaganza - PAPER". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "Wayback Machine" (PDF). web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ Harper, Todd; Adams, Meghan Blythe; Taylor, Nicholas (2018-10-19). Queerness in Play (kwa Kiingereza). Springer. ISBN 978-3-319-90542-6.
- ↑ Harper, Todd; Adams, Meghan Blythe; Taylor, Nicholas (2018-10-19). Queerness in Play (kwa Kiingereza). Springer. ISBN 978-3-319-90542-6.
- ↑ 17.0 17.1 "Let's Talk About Birdo – The Average Gamer". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.
- ↑ "The OutCrowd Spring 2018 by The OutCrowd Magazine - Issuu". web.archive.org. 2019-08-25. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-13.