Volga
(Elekezwa kutoka Volga (mto))
Volga (kwa Kirusi: Волга) ni mto mrefu kuliko yote ya Ulaya. Mwendo wake kuanzia chanzo hadi mdomo uko nchini Urusi. Urefu wake ni km 3,690. Inanaza kaskazini- magharibi ya Moskva na kupita kwenye tambarare za Urusi ya magharibi. Inaishia kwenye Bahari ya Kaspi kwa kimo cha -28 (chini ya UB) karibu na mji wa Astrakhan. Volga inapokea takriban mito 200 inayoishia humo.
Chanzo | vilima ya Valdai, mkoa wa Tver Oblast, Urusi |
Mdomo | Bahari ya Kaspi |
Nchi | Urusi |
Urefu | 3,692 km |
Kimo cha chanzo | 225 m |
Tawimito | mto Oka, mto Kama |
Mkondo | 8,060 m³/s (karibu na Volgograd) |
Eneo la beseni | 1,380,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Astrakhan, Volgograd, Samara, Kazan, Nizhny Novgorod, Yaroslavl |
Mto ni njia ya maji muhimu inayounganana na:
- Bahari ya Baltiki kupitia mfereji wa Volga-Baltiki
- Bahari Nyeupe kupitia mfereji wa Baltiki-Bahari Nyeupe
- Bahari Nyeusi na Mediteranea kupitia mfereji wa Volga-Don
Picha
hariri-
Rzev ni mji wa kwanza kwenye mwendo wa Volga. Picha ya mwanzo wa karne ya 20
-
Mto Volga karibu na Ulyanovsk
-
Picha kutoka angani
-
Volga ikifunikwa kwa barafu wakati wa Januari
Tazama pia
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Volga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |