François-Marie Arouet anayejulikana zaidi kwa jina la Voltaire alikuwa mwandishi na mtaalamu wa falsafa kutoka Ufaransa.

Voltaire
Jina la kuzaliwa François-Marie Arouet
Alizaliwa 21 Novemba 1694 (mjini Paris)
Alikufa 30 Mei 1778 (Paris)
Nchi Ufaransa
Kazi yake Mwanafalsafa

Anahesabiwa kati ya waanzilishaji wa Zama za Mwangaza nchini Ufaransa.

Alitetea uhuru wa mawazo na uhuru wa dini ingawa enzi zake sheria za Ufaransa zilikuwa kali na dini iliamriwa na serikali, kama ilivyokuwa katika nchi nyingi za Ulaya.

Kwa miaka 3 (kuanzia 1726 hadi 1729) aliondoka nchini na kuishi ugenini huko Uingereza ambapo mawazo yake yalikubalika zaidi. Inasemekana alikwenda akiwa msanii akarudi ni mwanafalsafa, akimfuata hasa Locke.

Baadaye alienda kuishi Berlin (Prussia, leo Ujerumani), halafu tena Uswisi. alipobaki mpaka karibu na kufa.

Aliandika mengi pamoja na tamthiliya, shairi na maigizo. Maandiko yake yaliathiri Mapinduzi ya Marekani na Mapinduzi ya Ufaransa ya 1789.

Voltaire alipinga mafundisho mengi ya Kanisa Katoliki na ya dini nyingine zinazodai kutokana na Ufunuo wa Mungu, akiziita ushirikina. Kwa namna ya pekee alipinga maandishi ya Blaise Pascal.

Badala yake akasimama upande wa imani ya Mungu asiyetambulika na asiye na uhusiano na binadamu akimwamini kuwa tu chanzo cha ulimwengu na namna ya nishati ndani yake.

Pia alijiunga na chama cha siri cha Umasoni.

Alipokufa hakuzikwa kanisani.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: