Voyager 1
Voyager 1 ni chombo cha angani kilichorushwa mwaka 1977 na shirika la NASA nchini Marekani kwa kusudi la kupeleleza anga-nje katika mfumo wa Jua letu hadi anga-nje kati ya nyota. Inaendelea kufanya kazi na kutuma data inayokusanya kwa kutumia vyombo vya upimaji ndani yake.
Chomboanga cha mbali kutoka Dunia
haririVoyager 1 ni chombo cha kutengenezwa na binadamu kilichofikia umbali mkubwa na Dunia yaani 145 vizio astronomia vinavyolingana na kilomita bilioni 21.6; nuru ya Jua inahitaji zadi ya masaa 20 kufikia Voyager 1 (hali ya Mei 2019).
Mwaka 2012 ilitembea nje ya mzingo wa Pluto katika kanda ya heliosferi penye mata ya mwisho inayoshikwa na graviti ya Jua ikiandaa kuondoka katika mfumo wa Jua letu kabisa na kuingia anga-nje kati ya nyota.
Voyager 1 ilipita karibu na sayari za Mshtarii na Zohali na kupiga picha za sayari hizi na miezi yao. Inaendelea kupima mnururisho uliopo angani na kutuma data duniani. Inachukua nguvu yake kutoka beteri zenye plutoni nururifu zinazozidi kufifia. Imekadiriwa kwamba kifaa cha mwisho kinachoweza kupima data kitazimika mwaka 2013.
Kupita mipaka ya mfumo wa Jua
haririVoyager 1 imeshapita katika Ukanda wa Kuiper ikieleka sasa kwenda wingu la Oort. Imeshapita eneo la heliosferi.
Voyager 1 inaendelea huko gizani na mwezi wa Mei 2019 ilifikia umbali wa km bilioni 21.6 au vizio astronomia (umbali kati ya Jua na Dunia) 145[1]. Bado inatuma data kuhusu uga sumaku ya Jua. Watafiti kutoka Ugiriki (Dialynas Kostas na wengine) walitumia data zake pamoja na Voyager 2 na Cassini kusema kumbe heliosferi ina umbo la tufe bila mkia mkubwa jinsi iliyoaminiwa awali.[2]
Picha za Mshtarii (Jupiter) zilizotumwa na Voyager 1
hariri-
Doa Kubwa Jekundu katika angahewa ya Mshtarii (Jupiter) jinsi ilivyoonekana kutoka Voyager 1.
-
Picha ya Io mwezi wa Mshtarii.
-
Picha ya angahewa ya Mshtarii ilivyopigwa na Voyager 1.
-
Kasoko la Valhalla kwenye mwezi Callisto wa Mshtarii ilivyopigiwapicha na Voyager 1 mwaka 1979.
Zohali (Saturn)
hariri-
Voyager 1 image of Saturn from 5.3 million km four days after its closest approach.
-
Layers of haze covering Saturn's satellite Titan
-
Titan's thick haze layer is shown in this enhanced Voyager 1 image.
-
Voyager 1 image of Saturn's F ring
Marejeo
hariri- ↑ Mission Status, tovuti ya voyager.jpl.nasa.gov (Jet Propulsion Labaroty, CALTECH, Marekani), iliangaliwa 3 Mei 2019
- ↑ [Nature.com/articles/s41550-017-0115 Hitimisho la utafiti wa Kostas]
Viungo vya nje
hariri- NASA Voyager website
- Voyager Spacecraft Lifetime — interstellar mission coverage.
- Spacecraft Escaping the Solar System Ilihifadhiwa 27 Aprili 2007 kwenye Wayback Machine. — current positions and diagrams
- CNN: "NASA: Voyager I enters solar system's final frontier", 25 Mei 2005
- CNN: "NASA: Voyager II detects solar system's edge", 25 Mei 2006
- Weekly Mission Reports — includes information on current spacecraft state
- [1] Trailer ya filamu ya 2017 "The Farthest", si ya kisayansi sana lakini picha nzuri