Wafiadini wa Eleutheropoli

Wafiadini wa Eleutheropoli ni askari Wakristo 50 hivi waliouawa na Waislamu huko, nchini Israeli, mwaka 638.

Majina yao ni pamoja na: akina Yohane 10, akina Joji 7, akina Teodori 5, akina Paulo 3, akina Sergio 2, akina Stefano 2, akina Zita 2, halafu Fotino, Eugeni, Museli, Teopempto, Siriaki, Filoseno, Teodosi, Epifani, Thoma, Kononi, Paulino, Kaiumas, Abramio, Marmises na Marino. Walikatwa kichwa kwa kukataa kusilimu.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 17 Desemba[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.