Wagoma (kwa Kigoma, au Ki'oma: Ba'ómà), ni kabila la Kibantu kutoka Mkoa wa Kigoma (wilaya ya Kigoma Mjini) na mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (jimbo la Kivu Kusini na wilaya ya Kalemi, eneo ambalo hapo zamani liliitwa Ugoma).

Idadi ya Wagoma haijulikani kwa vile ni kabila la watu wanaopenda kujificha sana na hujitambulisha zaidi kama Wamanyema.[1][2]

Historia hariri

Inasemekana wana asili ya Kaskazini mwa Afrika.

Inaelezwa takribani Wagoma wote walihama eneo la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa sababu mbalimbali, hususani wakati wa utawala wa Kongo ya Kibelgiji.

Ndilo kabila la kwanza katika makabila ya Kibantu waliowahi kuvuka Ziwa Tanganyika na la mwanzo kuishi eneo la Kigoma Mjini.

Wagoma walifuatiwa na makundi ya Waniakaramba ama Wakwalumona na Wabwari. Kisha Wakwalumona waliunganika miongoni mwa Wabwari na ndipo na wao wakajiita Wabwari na wakakaa Kaskazini mwa Wagoma, kabla yao wote kuhamia na kukaa Ujiji na maeneo yote ya karibu yake ambako hapo wakajiunga na kujiita Wamanyema.

Wagoma waliweza kuvuka kabla ya makundi mengine kwa kufanikiwa kutengeneza mitumbwi ya mti mmoja ambayo waliichonga kutokana na miti ya Mivule iliyokuwa inapatikana Milima ya Goma, Magharibi ya ziwa.

Marejeo hariri

  1. Burton, Richard F. (1860). The Lake Regions of Central Africa: A Picture of Exploration, Volume 1. Harper & Brothers Publishers: New York.
  2. Kigoma Development Association (Tanzania) 1994, p. 51.
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wagoma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.