Walanyama (pia: Wagwizi; kwa Kilatini: Carnivora) ni mpangilio wa kisayansi ambao hujumuisha aina zaidi ya 280 za wanyama wa ngeli ya mamalia (wanaonyonyesha wadogo wao)[1].

Dubu Kahawia, mmoja kati ya walanyama wakubwa zaidi.
Paka na mbwa, wanyama wa nyumbani ni walanyama.

Ukubwa wao unaanzia kwa vicheche wadogo kama (Mustela nivalis), mwenye gramu 25 na sentimeta 11, hadi dubu barafu (Ursus maritimus), ambaye anaweza kupima kilogramu 1,000, na Tembo-bahari wa kusini (Mirounga leonina), ambao wanaume wazima wanafikia kilogramu 5,000 (lb 11,000) na urefu wa mita 6.9 (futi 23).

Wengi wao hula nyama hasa, na ndiyo msingi wa jina la kundi "carnivora" (walanyama). Kuna pia spishi kama rakuni na dubu kadhaa ambao hula chochote, yaani nyama pamoja na matunda, jozi, nafaka na majani kadhaa. Spishi chache zimekuwa walamani kama vile Panda ambao ni dubu wanaokula mianzi pekee.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Flynn, J. J.; Finarelli, J. A.; Zehr, S.; Hsu, J.; Nedbal, M. A. (April 2005). "Molecular phylogeny of the Carnivora (Mammalia): Assessing the impact of increased sampling on resolving enigmatic relationships". Systematic Biology 54 (2): 317–37. doi:10.1080/10635150590923326 . PMID 16012099

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Walanyama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.