Wameru (Kenya)
Wameru ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi maeneo ya Meru, Kenya.
Kwa lugha yao, wanajiita "Wangaa" kutokana na jina la mwanzilishi wa kabila lao.
Wana uhusiano wa karibu na Wakikuyu, Waembu, na Wambeere, kumbe ni tofauti kabisa na Wameru wa Tanzania.
Mila
haririMajina ya urithi
haririKatika mila na desturi yao, jina ambalo mtoto atapewa huwa na kiambatanishi "mto...", kinachomaanisha "mtoto wa fulani na fulani". Kwenye maandishi, kiambatanishi hiki hufupishwa hadi M'. Kwa mfano, kama jina la mwana ni Kithiki, na la baba ni Mwenda, jina litaandikwa "Kithiki M'Mwenda", lakini kwa matamshi, ni "Kithiki Mto Mwenda"[1].
Marejeo
haririMakala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wameru (Kenya) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |