Warungu
Idadi ya watu wa Afrika ya Kati
Walungu ni kundi la makabila mawili ya Kibantu yaani Walungu wa Chifu Tafuna (Mambwe-Lungu) na Walungu wa Chifu Mukupa Kaoma (Malaila-Lungu). Mambwe Lungu, ambao ni lengo kuu la makala hii, wanapatikana hasa katika mwambao wa kusini-magharibi wa Ziwa Tanganyika katika Wilaya ya Kalambo ya Mkoa wa Rukwa, Tanzania, na kaskazini-mashariki mwa Zambia hasa katika wilaya ya Mpulungu na Mbala.
Mwaka wa 1987 idadi ya Walungu nchini Tanzania ilikadiriwa kuwa 34,000. Idadi ya Walungu nchini Zambia haijakadiriwa kwa kujitegemea, ingawa jumla ya idadi ya Mambwe na Lungu nchini Zambia ilikadiriwa kuwa 262,800 mwaka wa 1993.[1]
Kilungu, lugha ya Warungu, na Kimambwe ni lahaja za lugha moja.
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Warungu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |