Mkoa wa Rukwa ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 55000.

Mkoa wa Rukwa
Mahali paMkoa wa Rukwa
Mahali paMkoa wa Rukwa
Mahali pa Mkoa wa Rukwa katika Tanzania
Majiranukta: 7°0′S 31°30′E / 7.000°S 31.500°E / -7.000; 31.500
Nchi Tanzania
Wilaya 4
Mji mkuu Sumbawanga
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Joachim Wangabo
Eneo
 - Jumla 22,792 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 1,540,519
Tovuti:  http://www.rukwa.go.tz/
Mkoa wa Rukwa kabla haujamegwa upande wa kaskazini (2012).

Unapakana na mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi upande wa kaskazini, mkoa wa Mbeya upande wa mashariki, Zambia kusini na upande wa magharibi Ziwa Tanganyika lililo mpaka na Kongo pia.

Makao makuu ya mkoa ni Sumbawanga.

Kabla ya kumegwa mwaka 2012 eneo la mkoa lilikuwa takriban km² 70,000. Kwa sasa lina kilomita ya mraba 22,792.

Kusini mwa mkoa liko ziwa Rukwa ambalo ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki.

Wilaya

hariri

Wilaya ziko nne (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022 [1].):

Wilaya ya Mpanda ilikuwa sehemu ya Rukwa ikawa kiini cha mkoa mpya wa Katavi kuanzia mwaka 2012.

Wakazi

hariri

Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa wakazi 139,019 [2], kwa asilimia kubwa waumini wa Kanisa Katoliki.

Kabila kubwa zaidi mkoani ndio Wafipa walioko hasa katika wilaya za Sumbawanga na Nkasi. Kati ya makabila mengine kuna Wamambwe-Lungu, Wawanda na Wanyamwanga katika wilaya ya Sumbawanga; kuna pia Wasukuma, Wanyamwezi na Wamasai.

Majimbo ya bunge

hariri

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Rukwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.